Marufuku kutoka nyumbani Kyiv kwa saa 36 ngumu



Kyiv itaweka sheria kali kwa saa 36 kuanzia leo usiku kabla ya (wakati hatari na mgumu) baada ya mashambulizi kadhaa ya Russia, Meya Vitali Klitschko amesema.

Tangazo hilo limekuja wakati Russia ikianza mashambulizi katika mji huo mkuu wa Ukraine, ambao unakaribia kuzungukwa na wanajeshi wa taifa hilo la Mashariki katika wiki ya tatu ya uvamizi iliyoondoka na nusu ya maisha ya watu milioni 3.5 waliokuwepo kabla ya vita.

Leo ni wakati mgumu na hatari," alisema bingwa huyo wa zamani wa ngumi za uzito wa juu katika taarifa aliyoitoa mtandao wa Telegram.

Hii ndio sababu nawaambia wakazi wote wa Kyiv kujiandaa kutotoka nyumbani kwa siku mbili, au kama king'ora kitazima, mafichoni.

Amri hiyo ya kutotoka itaanza saa 2:00 jioni Jumanne hadi saa 1:00 jioni Alhamisi kwa mujibu wa amri ya jeshi, alisema.

Limekuja wakati mawaziri wakuu wa Poland, Czech na Slovenia walikuwa wakisafiri kwa treni leo kwenda Kyiv katika ziara ya kwanza ya viongozi wa nje kwenye mji huo mkuu.

Kyiv, Ukraine (AFP). 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments