Marufuku watoto chini ya miaka 9 kupanda bodaboda


Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoani Iringa, kimepiga marufuku watoto chini ya umri wa miaka tisa kupanda bodaboda.

Mkuu wa Kitengo hicho, ASP Yusuph Kameta amesema ni kosa kisheria kwa mtoto chini ya umri huo kupanda bodaboda.

Hata hivyo, wazazi na walezi wengi ndio wanaoongoza kuwapakia watoto wao kwenye usafiri wakati wa kwenda na kurudi shuleni bila kujali usalama wao.

“Ni marufuku, mtoto mdogo hawezi kuvaa kofia ngumu hata akivaa kabla hajaanguka chini, kofika inakuwa imeshafika. Ni hatari sana,” amesema Kamota na kuongeza;

“Mzazi unaachaje mtoto wako mdogo apande bodaboda? Halafu wengine wanawapakia mpaka watoto wawili au watatu bila kujali kabisa, likitokea lolote unapata misiba miwili.”

Amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wazazi juu ya kuwasaidia watoto wao ili badala ya kutumia usafiri huo watumie bajaji, daladala au mabasi ya shule.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi wamesema majukumu mengi yamekuwa yakichangia wengi kuona bodaboda kama njia rahisi ya usafiri kwa watoto wao.

“Mama wa watoto wangu yupo bize na mie ni dereva bodaboda ndio maana huwa nawapeleka mwenyewe, sikujua kama ni kosa,” amesema Jones Ngeli, mkazi wa Kihesa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments