Mbunge: Ubeberu na uzayuni zinataka kuigawa Morocco katika maeneo matano madogo

Mwakilishi wa Bunge la Morocco amesema kuwa, ubeberu na uzayuni zinafanya njama za kuigawa nchi hiyo katika maeneo matano madogo.

Bi Nabilah Munib, ametahadharisha kwa kusema kuwa, Morocco inakabiliwa na hatari kutoka nje kupitia kivuli cha ubeberu na uzayuni.

Ameongeza kuwa, pande hizo zimeilenga ardhi yote ya Morocco kwa njama na kwamba, wahusika hao ndio walioleta vurugu, machafuko na uharibifu mkubwa katika mataifa ya Afghanistan, Iraq, Yemen na Syria.

Mbunge huyo amesema kuwa, wananchi wa Morocco wanapaswa kuwa na umoja na mshikamano ili waweze kukabiliana na njama hizo.

Kadhalika Bi Nabilah Munib amesisitiza kuwa, kwa mujibu wa vituo kadhaa vya utafiti, Morocco inahitajia muelekeo mpya wa utaifa, uzalendo na kufanyika juhudi kwa ajili ya kuiondoa nchi hiyo katika mgogoro.


Imarati na Bahrain zilipotia saini ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel

 Wakati huo huo, Harakati ya Morocco ya Kuunga Mkono Palestina na Kupinga Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Israel hivi karibuni ililiandikia Bunge la Morocco barua ya wazi ikisisitiza himaya na uungaji mkono wake kwa wananchi wa Palestina.

Itakumbukwa kuwa, mwaka 2020 nchi nne za Kiarabu za Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati), Bahrain, Morocco na Sudan zilisaini hati za makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni, hatua ambayo imeendelea kupingwa na kulaaniwa vikali katika kila kona ya nchi za Kiarabu na Kiislamu na hata ndani ya nchi hizo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments