Rais Samia azindua mfumo utakaotatua ubambikaji bili za maji

Rais wa Samia Suluhu Hassan amezindua mifumo miwili ya Tehama inayowezesha ufuatiliaji wa miradi ya maji pamoja na ulipaji wa gharama za maji kwa wananchi.

Mifumo hiyo inalenga kuongeza ufanisi wa shughuli za wizara hiyo ikiwemo ufuatiliaji wa kina wa miradi ya maji.

Akieleza kuhusu mifumo hiyo Katibu Mkuu wizara ya Maji, Mhandisi Antony Sanga amesema wameianzisha ili kuongeza ufuatiliaji wa miradi na utoaji wa huduma za maji.

Amesema wataalamu wa ndani wametengenza Maji App ambayo itakusanya miradi yote ya maji na mtu yeyote anaweza kuiona kupitia simu janja.

“Kila mradi utaweza kuonekana kwenye simu ya mkononi kupitia Maji App ambayo itawezesha ufuatiliaji wake kwa ukaribu,”amesema mhandisi Sanga.

Mfumo mwingine ni wa utoaji wa bili za maji kwa mamlaka zote ambao umetajwa kuwa mwarobaini wa malalamiko ya wananchi kubambikiwa bili za maji.

“Kumekuwa na malalamiko ya wananchi kubambikiwa bili sasa tumekuja na mfumo huu wa tehama ambao utakuwa shirikishi katika kusoma bili na mwananchi anaweza kuripoti.

“Mfumo huu umeanza kufanya kazi na kwa kiasi kikubwa umepunguza malalamiko ya wananchi kuhusu kubambikiwa bili, sasa tunaupeleka Zanzibar nao wakanufaike na teknolojia hii”

Rais Samia aanika ugumu wa mradi wa maji Chalinze

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments