SAKHO AIWEZESHA SIMBA SC KUONGOZA KUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO


Na Alex Sonna

WAWAKILISHI Pekee ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Simba SC wameendelea kuwa tishio katika uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kuichapa bao 1-0 RSB Berkane ya Morocco katika Mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa jijini Dar es Salaam.

Shujaa wa Simba ni winga hatari Papa Sakho aliwanyanyua mashabiki wake dakika ya 44 baada ya kuichachafya ngome ya Berkane na kupiga shuti ndani ya kumi na nane na kumuacha Mlinda mlango hana la kufanya.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko pamoja kushambuliana kwa zamu huku Simba wakikosa nafasi nyingi za kufunga.

Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 7 na kuchupa hadi nafasi ya kwanza katika kundi D huku Berkane wakishuka nafasi ya pili wakiwa na Pointi 6,Nafasi ya tatu US Gendarmerie Pointi 4 na ASEC Mimosas wanashika nafasi ya mwisho wakiwa na Pointi 3.

Mchezo mwingine wa Kundi hilo utachezwa majira ya saa moja usiku ASEC Mimosas watakuwa nyumbani kucheza na US Gendarmerie

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments