SERIKALI YAWEKA MIKAKATI KUIMARISHA KILIMO NA MASOKO YA MAZAO YA VIUNGO VYA CHAKULA NA VIKOLEZO

    

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo(TARI) na Wakala wa Mbegu Tanzania(ASA) wametakiwa kuhakikisha wanafanya utafiti wa mbegu na kuzalisha mbegu kwa wingi za mazao ya viungo na vikolezo ili kuinuia tasnia ya mboga mboga na matunda nchini. 

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Anthony Mavunde wakati wa ziara ya kutembelea wilaya ya Arumeru,Arusha kujionea mashamba ya uzalishaji mbegu ya ngano,maharage na mazao ya mboga mboga na bustani yaliyopo maeneo ya Ngaramtoni na Tengeru pamoja na Kituo cha Utafiti wa Kilimo wa mazao ya mboga mboga na bustani-TARI Tengeru. 

“Serikali imedhamiria kuweka nguvu katika kuimarisha kilimo cha mboga mboga na bustani ili kitoe mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa letu,kutoka katika mauzo ya dola 750m kwa mwaka kufikia dola 2bn ifikapo mwaka 2030. 

Mh Rais Samia Suluhu Hassan ameifungua nchi kwa kuitangaza kimataifa hali itakayopelekea kupatikana kwa masoko ya uhakika ya mazao yetu ya mboga mboga na matunda. 

Lazima uzalishaji wa miche bora ya matunda na mbegu bora za mboga mboga uongezeke kutoka uzalishaji wa sasa ili tuweze kufikia malengo haya ya soko la kimataifa. 

TARI hakikisheni mnafanya utafiti wa kutosha katika eneo la viungo na vikolezo,eneo hili lina fursa nyingi sana lakini bado halijafanyiwa utafiti wa kutosha ili tuweze kuzalisha aina mbalimbali za mbegu bora za viungo kwa ajili ya soko la kimataifa,serikali inatambua umuhimu wa utafiti ndio maana bajeti katika eneo hili imeongezeka kufikia 11.7 bn kufikia 2022. 

Kwa ASA hakikisheni mnaongeza uzalishaji wa miche mingi zaidi na mbegu bora za kuwezesha wakulima kulifikia soko la kimataifa,shirikisheni sekta binafsi na hasa Chama cha Wadau wa Viungo na Vikolezo ili kutambua mahitaji ya soko na aina gani za mbegu zizalishwe kwa uwingi kwa kwa wakati huu”Alisema Mavunde 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti,Watendaji wa *ASA* na TARI* wameahidi kufanyia kazi maelekezo hayo kwa uharaka ili kukuza tasnia ya mboga mboga na matunda na hasa katika eneo hilo la viungo na vikolezo.
 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments