UTEUZI: MCHECHU AREJEA NHC, POLEPOLE BALOZI MALAWI, ULANGA BOSS MPYA TTCL





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi
kama ifuatavyo:

i. Amemteua Bwana Waziri Kindamba Waziri kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Bwana Kindamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) anachukua nafasi ya Mhandisi Marwa Mwita Rubirya ambaye amestaafu kwa umri.

ii. Amewateua Bwana Humphrey Hezron Polepole kuwa Balozi wa Tanzania Nchi ya Jamhuri ya Malawi na Mhe. Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 Ibara ya 67(2) (g) ikisomwa pamoja na Ibara ya 71(1)(a).

iii. Amewateua Balozi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (Mstaafu) Ernest Jumbe Mangu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari (Tanzania Port Authority) na Meja Jenerali John Julius Mbungo, Mkurugenzi Mstaafu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Meli Tanzania (MSCL).

iv. Amemteua Bwana Peter Rudolph Ulanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (Tanzania Telecommunication Corporation Limited – TTCL) na Bwana Nehemia Kyando Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing Corporation). Bwana Ulanga ni Mkurugenzi Mstaafu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) na Bwana Mchechu aliwahi kutumikia Shirika la Nyumba (NHC) huko nyuma kwa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na anachukua nafasi ya Dkt. Maulid Banyani, atapangiwa kazi nyingine.

Bw. Kindamba na Balozi Mteule Polepole wataapishwa tarehe 15 Machi, 2022 saa 04:00 asubuhi viwanja vya Ikulu, Chamwino, Dodoma.
Uteuzi huu unaanza mara moja.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments