Vijana wazindua mfumo wa kurahisisha kupata ajira

Vijana wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Kiislamu Tanzania (Tampro), umezindua mfumo wa kuomba ajira mtandaoni utakaowarahisishia wenzao kutafuta ajira kwa urahisi katika taasisi mbalimbali zikiwemo za sekta binafsi.

Mfumo huo umebuniwa na vijana wa Tampro ili kurahisisha watu wa kuona fursa za ajira zilizopo katika taasisi na kampuni mbalimbali kwa njia ya mtandao.

Ubunifu huo umezinduliwa leo, Jumapili Machi 27, 2022 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk Seleman Jafo aliyewapongeza vijana hao na uongozi wa Tampro kwa hatua hiyo, akisema wametumia maarifa na ujuzi katika kufanikisha mchakato.

Mussa Kiwele mmoja wa wabunifu wa mfumo huo, amesema ili kuutumia mchakato huo lazima kijana ajiandikishe kwa njia ya barua pepe, kisha kujibiwa papo hapo, baada ya hapo mwombaji ataruhusiwa kutengeneza au kuweka wasifu wake pamoja na vyeti vya shule na vyu alivyosoma.

“Baada ya hapo atapata nafasi ya kuona matangazo ya kazi kutoka taasisi au kampuni mbalimbali kisha ataruhusiwa kuomba kazi. Kulingana na kazi alioomba mwombaji atakuwa anasubiri majibu ikiwemo kuingizwa katika orodha ya usajili au la,” amesema Kiwele.

Naye, Waziri Jafo amesema, “baadhi ya vijana walikuwa wanapata taarifa za matangazo ya ajira kupitia magazeti na makundi ya mitandao ya kijamii. Lakini mfumo huu utatufungulia nafasi nzuri ya kwa vijana ya kuandaa taarifa zao na kuzituma sehemu husika,” amesema Jafo.

Mwenyekiti wa Tampro, Haji Mrisho alisema mfumo huo, utawasaidia na kuwawezesha vijana kupata taarifa za ajira zitakazowaunganisha wadau mbalimbali zikiwemo  taasisi au kampuni binafsi.

By Bakari Kiango;Dar es Salaam.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments