Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Machi 15,

 LEO Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa Shilingi 2287.001 na kuuzwa kwa Shilingi 2309.9.

YUAN ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.34 huku ikiuzwa kwa shilingi 362.842 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.42 na kuuzwa kwa shilingi 19.58.
Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 151.64 na kuuzwa kwa shilingi 153.12 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.04 na kuuzwa kwa shilingi 20.20.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Machi 15, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Aidha,kwa mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 2982.72 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3013.47 na Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2504.50 na kuuzwa kwa shilingi 2530.47.
Wakati huo huo, Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.22 na kuuzwa kwa shilingi 2.28 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.61 na kuuzwa kwa shilingi 0.64.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments