Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Machi 22, 2022

LEO Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 153.15 na kuuzwa kwa shilingi 154.64 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.001 na kuuzwa kwa shilingi 20.2.


Dola ya Australia (AUD) inanunuliwa kwa shilingi 1687.63 na kuuzwa kwa shilingi 1705.43 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.061 na kuuzwa kwa shilingi 50.505.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Machi 22, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa Shilingi 2287.1 na kuuzwa kwa Shilingi 2309.94.
Aidha,kwa mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3003.151 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3034.11 na Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2521.95 na kuuzwa kwa shilingi 2548.1.

Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.9 huku ikiuzwa kwa shilingi 363.4 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.191 na kuuzwa kwa shilingi 19.380.

Wakati huo huo, Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.21 na kuuzwa kwa shilingi 2.28 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.61 na kuuzwa kwa shilingi 0.64.
Kwa mujibu wa Benki Kuu, Dirham (AED) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inanunuliwa kwa shilingi 622.74 na kuuzwa kwa shilingi 628.812 huku sarafu ya Austria ya Schilling (ATS) ikununuliwa kwa shilingi 146.8 na kuuzwa kwa shilingi 148.062.
 
NA GODFREY NNKO

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments