Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Kalisti Lazaro akizungumza na baadhi ya waendesha bodaboda Wilayani humo. Picha na Raisa Said |
Wito huo umetolewa leo Jumatano Machi 16, 2022 na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto (DC), Kalisti Lazaro alipokuwa akizindua Chama cha Bodaboda wilayani humo.
Amesema kuwa usajili wa chama utawapa uwezo wa kutumia fursa ya mikopo kutoka halmashauri na taasisi za fedha kama benki badala ya kuteseka na mikopo kandamizi.
Lazaro amezindua Chama cha Umoja wa Waendesha Pikipiki Wilaya ya Lushoto (Uwapilo) ambacho kina wanachama 4,200.
Awali, akisoma risala kwa niaba ya umoja huo, Katibu wa Uwapilo, Mwema Jacob alisema ukosefu wa mikopo kutoka Halmashauri na taasisi nyingine za fedha ni mojawapo ya changamoto kubwa inayowasababisha kutegemea kuajiriwa au kuingia katika mikataba kandamizi.
Jacob alisema kuwa walikuwa wanaingia mikataba kandamizi na wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa leseni za udereva na mafunzo ya usalama barabarani.
Waliomba vituo vya bodaboda na waendesha bodaboda kusajiliwa katika mfumo maalumu wa kanzi data wa Taifa na usajili huo uwasilishwe kwa mkurugenzi wa Halmashauri.
0 Comments