Wafanyakazi wanawake Tanesco watoa hamasa kwa wanafunzi wa kike ATC


Kuelekea siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limewapa hamasa wanafunzi wa kike wanaosoma masomo ya Ufundi katika Chuo cha ufundi Arusha (ATC),kuwa na nidhamu na uadilifu ili waweze kufikia ndoto zao.

Leo Machi 5,2022 baadhi ya wawakilishi wa wanawake wanaofanya kazi Tanesco kutoka mikoa mbalimbali wakiwemo waliosoma chuoni hicho wamekutana na wanafunzi hao.

Mbali ya kukutana na wanafunzo hao wa kike, Shirika hilo limekabidhi msaada wa Tool box 10 kwa ajili ya chuo hicho ili kuongeza zana za kujifunzia.

Wakitoa shuhuda baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo ambao wengine wamesoma chuoni hapo wamewaeleza wanafunzi hao kuwa ili waweze kutimiza ndoto zao na kupata mafanikio ni lazima waongeze nidhamu na kuwa waadilifu.

“Ninawatia moyo kuwa kila kitu kinawezekana mkimtanguliza Mungu, nidhamu,heshima na kuwa waadilifu kwani kwa maendeleo endelevu ya kizazi hiki ni lazima wanawake mpende masomo ya sayansi,”amesema Meneja wa Tanesco,Kinondoni Kaskasini,Regina Mvungi

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Maharage Chande, Mhandisi Sophia Mgonja, amesema lengo lao kutembelea chuo hicho ni kutoa hamasa kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya ufundi ikiwemo sayansi chuoni hapo ili kubadili dhana ya kuwa masomo ya sayansi ni magumu kwa wasichana.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amelipongeza shirika hilo kwa hamasa waliyotoa kwa wanafunzi hao wa kike na kuwa kupitia hamasa hiyo itasaidia wanafunzi hao wasikate tamaa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments