WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI MKOA WA DAR ES SALAAM WAPEWA ELIMU KUHUSU VIWANGO NA TBS

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Bi.Viola Masako akifungua mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari uliyofanyika leo Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Bw.Lazaro Msasalaga akizungumza katika mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari uliyofanyika leo Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Uandaaji Viwango (TBS) Mhandisi Yona Afrika akizungumza katika mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari uliyofanyika leo Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam. Afisa Habari na Mawasiliano TBS, Bi.Neema Mtemvu akizungumza katika mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari uliyofanyika leo Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.Baadhi ya watumishi wa TBS na Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari uliyofanyika leo Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Bi.Viola Masako akipata picha ya pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari uliyofanyika leo Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.


Shirika la Viwango Tanzania –TBS limewataka wanahabari kutumia kalamu zao kuwasisitiza wataalamu mbalimbali kuwa uandaaji wa viwango ni wa shirikishi bila kikomo kwani lengo ni kutoa uhakikisho wa ubora,usala ma,kuaminika na ufanisi.

Hayo yamejiri leo jiji Dar es salaam katika mkutano baina ya Shirika hilo na wahariri wa vyombo vya habari ambapo imeelezwa kuwa wanahabari wakatapokuwa na uelewa wa masuala mbalimbali yahusuyo TBS itasaidia kurahisisha kufikisha elimu kwa jamii namna bora ya masuala ya viwango.

Akizungumza wakati akifungua Mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBS,Kaimu Mkurugenzi Mkuu Viola Masako amesema kuifahamu elimu ya viwango ina faida mbalimbali ikiwemo kuipa serikali urahisi wa kuunga sheria zinazohusiana na masuala ya afya,usalama na uhifadhi wa mazingira.

Akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa ushiriki katika mchakato wa uandaaji viwango,Meneja wa Viwango Yona Afrika amefafanua kuwa kiwango kinapokuwa cha kitaifa utekelezaji wake ni mwananchi yeyote huku akizitaja faida za viwango kuwa ni pamoja na urahisishaji wa biashara.

‘Faida nyingine za viwango hulinda afya na usalama wa walaji/watumiaji wa bidhaa mbalimbali lakini pia huondoa mkanganyiko kuhusiana na bidhaa’amesema Yona

Kwa upande wake Mnja wa Upimaji TBS Joseph Makene akiwasilisha mada kuhusu huduma zitolewazo na kurugenzi ya upimaji na ugezi amesema vifaa vinavyotumika katika maabara zilizopo katika Shirika hilo ni vya kisasa na vinatumia teknolojia ya kisasa.

Hata hivyo imeelezwa kuwa TBS pia hutoa huduma ya kuratibu na kuthibitisha ubora wa biadhaa kwa kutumia viwango vya kampuni,vya kigeni au vya kimataifa vilivyothibitishwa na kamati maalum hususani pale ambapo hakujawa na kiwango cha kimataifa cha bidhaa husika.
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments