Wajue mawakili waliokuwa wakiwatetea kina Mbowe

Kesi ya ugaidi iliyokuwa ikimkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ambao ni makomandoo walioachishwa jeshini jana Ijumaa, Machi 4, 2022 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) amewafutia mashtaka katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

DPP amewasilisha taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao (Nolle Prosequi) kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), wakati washtakiwa hao wakitarajiwa kupanda kizimbani kujitetea kufuatia uamuzi wa Mahakama.

Katika kesi hiyo namba 16 ya mwaka 2021, washtakiwa hao walikuwa wakitetewa na jopo la mawakili wengi ambao walipambana kwa hoja mbalimbali kuhakikisha kuwa wanawachomoa katika kadhia hiyo.

Wakati kesi hiyo inaanza kusikilizwa mahakamani hapo Agosti 31, 2021 mawakili wote walikuwa wakiwakilisha washtakiwa wote kwa pamoja, lakini baadaye waliamua kujigawa na kugawana washtakiwa na kila mshtakiwa akawa na mawakili wake pekee, japo walikuwa wakishirikiana kutokana na kuwa na maslahi sawa.

Jeremiah Mtobesya: Wakili wa kujitegemea, amewahi kusimamia kesi mbalimbali za jinai na za madai, zikiwemo za dawa za kulevya zilizokuwa zikiwakabili, raia wawili wa kigeni

Ameshasimia kesi mbalimbali za aina tofautitofauti, yeye mwenyewe, au akiwa miongoni mwa mawakili waliokuwa wakiunda majopo ya utetezi katika kesi hizo.

John Mallya: Ni wakili wa kujitegemea ambaye katika kesi hii alikuwa akimtetea mshtakiwa wa pili, Adamu Hassan Kasekwa, maarufu kama Adamoo. Ni wakili ambaye amekuwa akitumia maswali ya uchokozi.

Katika kesi hiyo alikuwa akimtetea mshtakiwa wa tatu, Mohamed Abdillahi Ling’wenya

Ameshasimamia kesi nyingi za madai za jinai zikiwemo kesi mbalimbali za viongozi wa Chadema na za watu binafsi ikiwemo kesi ya hivi karibuni ya msanii Menina Abdulkarim Atiki. Ni wakili wa kujitegemea na mmoja wa mawakili wanaounda jopo la mawakili wa utetezi katika kesi hiyo.

Dickson Matata: Ni wakili wa kujitegemea aliyekuwa akimsimamia mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo, Mohamed Abdillahi Ling’wenya, akisaidiana na Wakili Fredrick Kihwelo

Alilazimika kusomea sheria ili kutetea haki za watu mbalimbali wanaodhulumiwa, baada ya kukutana na madhila ya askari wa Jeshi la Magereza alipokwenda kumuona ndugu yake aliyekuwa mahabusu, katika gereza la Uyuyi, Tabora.

Amewahi kusimamia kesi mbalimbali za jinai na za madai. Miongoni mwake ni pamoja na kesi yeye mwenyewe na nyingine akiwa miongoni ma mawakili waliokuwa wanaunda majopo ya mawakili wakiwatetea viongozi wa Chadema, zikiwemo za Uchochezi zilizokuwa zikimkabili Makamu mwenyekiti Chadema, Tundu Lissu.

Fredrick Kihwelu: Ni wakili wa kujitegemea ambaye amekuwa akisimamia kesi mbalimbali za madai na za jinai zikiwemo za viongozi wa Chadema wa ngazi mbalimbali.

Katika kesi hii ya ugaidi iliyokuwa ikiwakabili kina Mbowe alikuwa akimtetea mshtakiwa Ling’wenya akishirikiana na wakili Matata.

Peter Kibatala: Wakili wa kujitegemea, amewahi kuwa Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Katika majukumu ya uwakili ameshasimamia kesi mbalimbali za jinai na za madai, ikiwemo za viongozi mbalimbali wa Chadema.

Pia alikuwa mmoja wa mawakili na aliyehusika sana katika kesi ya muigizaji maarufu wa filamu wa kike nchini, Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu.

Miongoni mwa kesi nyingi anazoendelea kuzisikliliza ni pamoja na kesi ya mauaji inayomkabili mke aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, Erasto Msuya, maarufu kama Bilionea Msuya; Miriam Mrita na mwenzake, Revocatus Myella.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments