Ni miezi tisa imepita tangu wananchi wa kijiji cha Gabimori kata ya Kyangasaka wilaya ya Rorya mkoa wa Mara kukosa huduma ya maji ya bomba baada ya mashine ya kusukuma maji kutoka kwenye chanzo cha maji kuharibika hali iliyowalazimu kutembea umbali wa km 3- 5 kufuata maji Ziwa Victoria.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari waliotemblea mradi wa maji wa Gabimori ,Mwenyekiti wa mradi wa maji katika kijiji hicho Said Mabele alisema kuwa mradi wa maji ulikamilika 2017 na kutoa maji lakini Februari,2021 ulistisha hudumalakini kwa sasa mradi huo umeboreshwa na kutoa huduma ya maji.
"Mradi uliharibika inveta ilisheki kule kwenye chanzo cha maji,betri ilikuwa inaharibika kila mara ilibidi watu wakachote maji ziwani umbali wa km3-5 kutegemea na umbali anakoishi,tukawajulisha RUWASA wakatutengenezea mfumo mzuri mashine inasukumwa kutumia Sola(Nishati ya jua) sasa hivi maji yanapatikana muda wote,sisi tunatengeneza matengenezo yale madogomadogo yale makubwa RUWASA ndiyo wanayashughulikia.
"Kata ina vijiji viwili cha Kyangasaka na Gabimori mradi unahudumia zaidi ya kaya 600,ndoo moja ya maji ni sh.50 hadi sasa tuna fedha kwenye akaunti sh.499,000,fedha hizo ni kwa ajili ya kuzitumia kwenye matengenezo pindi kunapotokea tatizo kama mabomba kupasuka, bila wananchi kuchota maji hatutapata fedha za matengenezo,tunaomba na vitongoji ambavyo havijafikiwa na maji navyo vipate maji yasambazwe kwakuwa mashine ipo haina tatizo ",alisema Said.
Fundi mradi Nyabimori Marwa Matare alisema”kuna changamoto ya vifaa vya mradi kuharibika ukiweka vifaa umbali wa mita moja ni sh.75,000 na gharama uongezeka kadri ya umbali ulivyo, mabomba yanapasuka mara kwa mara tunaendesha mradi kwa kutumia sola mvua ikinyesha maji yanakuwa ya kusuasua ,sola zipo 44 kila sola moja ina watsi 260 mashine inayosukuma maji kwenda kwenye tenki ni ya kisasa.
Na Dinna Maningo,Rorya.
0 Comments