Wasiwasi wa Umoja wa Afrika kuhusu kubaguliwa Waafrika nchini Ukraine

Umoja wa Afrika umebainisha wasiwasi Jumatatu kuhusu ripoti kwamba Waafrika huko Ukraine wanabaguliwa na wanazuiliwa kuvuka mpaka ili kukimbia vita vinavyoendelea katika nchi hiyo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais wa Senegal Macky Sall na mwenyekiti wa tume ya umoja huo Moussa Faki Mahamat wamesema katika taarifa ya pamoja kwamba wanakerwa na ripoti hizo.

"Ripoti kwamba Waafrika wanabaguliwa ni ya kushangaza kwani huo ni ubaguzi wa rangi na ni uvunjaji wa sheria ya kimataifa," imesema taarifa hiyo.

Nigeria imebainisha kusikitishwa na ripoti kwamba Wanigeria wanabaguliwa na maafisa wa polisi nchini Ukraine wakati wakijaribu kukimbia vita.

Waziri wa Mambo ya Nje Geoffrey Onyeama amesema Wanigeria wengi ambao wamefanikiwa kukimbia Ukraine wamelalamika kuwa wanakabiliwa na ubaguzi wa aina fulani na polisi wa mpaka wa Ukraine

Amesema kuna takribani raia 8,000 wa Nigeria nchini Ukraine na kwamba baadhi yao wamefanikiwa kufika katika balozi za Nigeria katika nchi jirani. Ameongeza kuwa mipango inaendelea kwa ahili ya kuwaondoa nchini humo raia wengine wa Nigeria.

"Romania itakuwa kitovu cha uokoaji," amesema katika mahojiano.

Waafrika, wakiwemo wanawake wenye watoto Ukraine wanabaguliwa na kuzuiwa kuondoka vitani huku Wazungu wakipewa kipaumbele

Mitandao ya kijamii imejaa klipu za video zikionyesha namna maafisa wa polisi wa Ukraine wanavyowazuia Waafrika kupanda treni kukimbia vita. Hata wanawake Waafrika wenye watoto wadogo wameonekana wakizuiwa kuondoka huku wazungu wakipewa kipaumbele. Hii ni pamoja na kuwa utawala wa Ukraine umekuwa ukisema wanawake wote wanapaswa kuruhusiwa kuondoka.

Oparesheni za kijeshi za Russia nchini Ukraine zilianza Alkhamisi iliyopita kufuatia amri ya Rais Vladimir Putin wa Russia na baada ya kuwa ametambua uhuru wa maeneo ya Donbass yaliyotangaza kujitenga na Ukraine. Putin alisema kwamba jeshi la nchi hiyo limeanzisha "operesheni maalumu ya kijeshi" hiyo kwa lengo la kuiondoa Ukraine katika hali ya kijeshi na kwamba Moscow haina nia ya kuvamia ardhi ya nchi hiyo.  

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments