Watu watatu wauawa Kigoma

              

Watu watatu wamefariki dunia baada ya kushambuliwa na wananchi wenye silaha za jadi katika katika kijiji cha Kagerankanda Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Machi 7, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma, James Manyama kati ya waliouawa mmoja ni raia kutoka nchi ya jirani Burundi.

Amesema kwa upelelezi wa awali unaonesha kuwa yalijitokeza matukio matatu ya ubakaji ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Makere ambapo wananwake watatu wakiwa wakitafuta kuni na uyoga walibakwa.

Amesema kuwa baada ya wanawake hao kubakwa, uongozi na wananchi wa kijiji cha Kagerankanda walifanya msako kwenye msitu huo na kuwakamata watu hao wawili waliokuwa wakifanya shughuli za kilimo katika hifadhi hiyo.

“Mara baada ya kuwakamata walianza kuwashambulia na silaha za jadi sehemu mbalimbali za miili yao   na kupelekea vifo vyao na kuwatuhumu kuhusika na vitendo vya ubakaji na baada ya kumaliza tukio hilo walitelekeza miili hiyo hapo hapo porini,” amesema Kamanda Manyama.

Kamanda Manyama amesema kuwa kutokana na mauaji hayo, Jeshi la polisi linawashikilia wananchi 15 akiwemo mwenyekiti wa kijiji hicho.

Amesema jeshi la polisi linaendelea na msako kuwabaini wote waliohusika na matukio hayo huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments