Watu wenye silaha washambulia mgodi na kuua watu 11 Burkina Faso

Burkina Faso ina utajiri mkubwa wa madini yakiwe dhahabu lakini wanaofaidika ni madola ya kibeberu hasa Ufaransa

Vyombo vya habari vimeripoti habari hiyo na kumnukuu mkazi mmoja wa eneo hilo akiliambia shirika la habari la AFP kwamba watu wasiojulikana wenye silaha wamefanya shambulio hilo kwenye mgodi wa madini ya dhahabu katika eneo la Baliata.

Alkhamisi wiki iliyopita pia watu 14 waliuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia mgodi wa dhahabu katika mji Seytenga wa jimbo la Séno la kaskazini mwa Burkina Faso.

Mwishoni mwa mwezi uliopita wa Februari kulitokea mripuko mkubwa karibu na mgodi wa dhahabu ulioko kusini magharibi mwa Burkina Faso na kuua watu 59 na kujeruhi wengine zaidi ya mia moja. Mripuko huo umetokea katika ghala la mada za kemikali zinazotumiwa kusafishia madini ya dhahabu. 

Burkina Faso ina utajiri mkubwa wa madini yakiwe dhahabu lakini wanaofaidika ni madola ya kibeberu hasa Ufaransa

Sansan Kambou ambaye ni mlinzi wa mazingira aliyekuwepo eneo la tukio hilo alisema maiti nyingi za watu zilitapakaa huku na kule. Watu walioshuhudia wamesema kukwa miripuko kadhaa ilisikika kwa kufuatana katika eneo hilo. 

Burkina Faso ina kasi kubwa ya uzalishaji wa madini ya dhahabu barani Afrika na kwa sasa inashika nafasi ya tano katika uzalisha wa madini hayo.

Karibu watu milioni 1.5 wanafanya kazi katika sekta ya madini ya dhahabu nchini Burkina Faso na mapato ya madini hayo yenye thamani kubwa na yanayopendwa sana duniani kwa mwaka 2019 ilitangazwa kuwa ni karibu dola bilioni 2. 

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments