Aliyetoa Eneo Kwa Ajili Ya Mradi,Kufikishiwa Maji Kabla Ya Mwenge Kuondoka Njombe

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndugu.Sahili Geraruma ameagiza halmashauri ya wilaya ya Njombe kumfikishia huduma ya maji mwananchi wa kijiji cha Ninga aliyetoa eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo kabla Mwenge haujaondoka katika mkoa wa Njombe.


Geraruma ametoa agizo hilo wilayani Njombe mara baada ya kukagua na kuzindua mradi huo wenye gahalama inayokadiliwa kufikia zaidi ya shilingi milioni 361 mapaka kukamilika kwake.

“Mwananchi aliyejitolea eneo lake kwa ajili ya mradi huu afikishiwe maji mpaka nyumbani kwake na utekelezaji huo ufanyike kabla Mwenge wa Uhuru haujaondoka mkoa wa Njombe,kabla sijaondoka nipate taarifa yule mwananchi ananufaika na maji nyumbani kwake kwa kutoa eneo hili”alisema Geraruma

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili kutokausha vyanzo katika maeneo yao na kusaidia upatikanaji wa maji kwa wakati wote.

Mbunge wa jimbo la Lupembe bwana Edwirn Swale ameshukuru Mwenge wa uhuru kwa kuzindua mradi huo utakaosaidia wananchi wa Ninga kupata huduma ya maji.

“Kwa niaba ya wananchi wa Ninga tunaomba utufikishie salamu kwa Mh.Rais kwamba wananchi wa Ninga wamefurahi sana kwa kuapata mradi huu wa maji”alisema Swale

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ameahidi kutekeleza agizo hilo kabla ya Mwenge wa Uhuru kuondoka mkoani humo.


Aliyetoa eneo kwa ajili ya mradi,kufikishiwa maji kabla ya Mwenge kuondoka Njombe

Kiongozi wa Mbio za Mwenge akimtwisha maji Mama wa kijiji hicho baada ya uzinduzi ikiwa ni ishara ya upatikanaji wa maji katika kijiji chao.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge akikata utepe katika moja ya kituo cha maji kwenye kijiji cha Ninga.

 Mradi wa maji uliozinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge.
 Na Amiri Kilagalila,Njombe

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments