Bulaya Ataka Mkakati Uendeshaji ATCL

             

Mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya ameshauri Serikali kuandaa mkakati wa kibiashara wa uendeshaji wa Shirika la Ndege Nchini (ATCL) na kulipa madeni ya ndani na nje ya nchi ili liweze kuzalisha faida.

 Bulaya ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 12, 2022 wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2022/2023.

Amesema katika hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu, imesema kuwa watanunua ndege za Serikali zifike 16 ni jambo jema na hakuna mtu anapinga hilo.

Hata hivyo, amehoji kama kununua pekee ni kulifufua na kama kuna mipango madhubuti ya uendeshaji kibiashara.

“Mwaka 2016 wakati tunalifufua shirika hili likiwa na ndege mbili za Bombadia ilikuwa na mtaji hasi wa Sh146 bilioni lakini leo lina mtaji hasi Sh242 bilioni,”amesema.

Amesema ukilinganisha mtaji na madeni ya takribani bilioni 371 haviendani na kwamba hali ya shirika ni mbaya.

Ameshauri kuwa shirika hilo lifanyiwe utaratibu liweze kujiendesha kwa kulipa mtaji na kuandaa mkakati wa kuliwezesha kujiendesha.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments