DC Iringa apiga marufuku kupandisha bei ya vyakula mwezi wa Ramadhan

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mohamed Moyo amepiga marufuku wafanyabishara kupandisha bei za vyakula wakati huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Moyo amepiga marufuku baada ya kufanya ziara ya ghafla katika soko kuu la Manispaa ya Iringa ili kuona bei za vyakula.

 “Sio mpandishe bei ya vyakula kwa sababu tu ni mwezi Mtukufu wa Ramadhani, uzeni kwa bei halali bei ambayo mlikuwa mnauza tangu awali,” amesema Moyo.

Amewataka Wakala wa Vipimo Manispaa ya Iringa kupita kwenye soko hilo ili kuona namna wateja wanavyopimiwa vyakula.

“Kuna watu wanaweka vyakula kama tambi kwenye vifungashio lakini ukipima utashangaa haifiki kilo moja au nusu kilo kama wanavyosema. Piteni mpime ili wananchi wasiibiwe,” amesema  Moyo na kuongeza;

“Nimepima hizo tambi walizosema ni nusu kilo nikagundua ni chache zaidi, hiki kitu hakikubaliki.”

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wamesema baadhi ya vyakula kama matunda vimepanda kutokana na gharama kubwa ya usafirishaji.

“Kuna bidhaa zilipanda kabla ya mwezi wa Ramadhani kwa hiyo wasione kama tumepandisha, tukiuza kwa bei ndogo ni hasara,”amesema.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments