Miongoni mwa mabadiliko yaliyofanywa na mkutano mkuu maalumu ni uchaguzi wa Abdulrahman Kinana kuwa makamu mwenyekiti chama hicho CCM (Bara) na mabadiliko ya katiba ya chama yaliyolenga kuimarisha utendaji.
Katika Mkutano huo, Kinana alipata kura zote za ndiyo kutoka kwa wajumbe 1,875 wa mkutano huo na kurithi mikoba ya Mzee Philip Mangula aliyeomba kung’atuka kwenye wadhifa huo.
Dewji alieleza furaha yake, akimtaja Kinana kuwa ni mtu makini na anayejua siasa.
“Nimefurahishwa na uteuzi wa Kinana pamoja na mabadiliko ya baadhi ya vifungu kwenye katiba ya chama.
Alisema kurejea kwa Kinana ni faraja sana, akikumbuka mwaka 2013-2014 alipotembea nchi nzima kukijenga chama hicho, hatua aliyosema ilirudisha imani upya kwa wanachama.
Akizungumzia mabadiliko ya katiba ya CCM ambayo yalipitishwa kwenye mkutano huo, Dewji alisema yamekuja kwa wakati mwafaka na moja ya maeneo yaliyomfurahisha ni mameya wa manispaa, majiji na wenyeviti wa halmashauri kupendekezwa na Kamati Kuu ya CCM badala ya madiwani kama ilivyokuwa hapo awali.
Alisema uamuzi huo utasaidia kudhibiti rushwa kwenye uchaguzi.
Kwa mujibu wa Dewji hapo awali watu wengi walikuwa wanatamani kuwa madiwani ili kupata fursa za kuwa meya na uchaguzi wao ulihusisha matumizi makubwa ya pesa kwenye baadhi ya maeneo.
“Hili ni jambo jema sana na muhimu na sasa rushwa itapungua…watu walikuwa wanashindana nani anatoa zaidi. Sasa unapogharamia kupata umeya ni lazima utakwenda kufanya mambo ambayo ni kinyume na matarajio ya wananchi,” alisema Dewji.
0 Comments