Dk. Mpango Ahimiza Wananchi Kutunzaji Na Kuhifadhi Mazingira

Makamu wa Rais Dk Philip Mpango awahimiza wananchi kushiriki katika suala la uhifadhi na utunzaji wa mazingira hapa nchini.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumamosi Aprili 2, 2022 wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa katika Uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe.

Amesema uhifadhi na utunzaji wa mazingira ni moja ya viipaumbele muhimu vya Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema suala la usafi linapaswa kuwa la kudumu hivyo wananchi wanatakiwa kushiriki katika kutunza mazingira.

Amesema bonde la mto Ruaha Mkuu unakabiliwa na changamoto mbalimbali za uharibifu wa mazingira na hivyo kuathiri mfumo wa ikolojia ambapo hali hiyo inatajwa kuathiri mipango mikubwa ya maendeleo yanayotegemea bonde hilo ikiwemo mradi wa kimkakati wa bwawa la kufufua umeme la Julis

Vilivile Mkuu wa mkoa wa Njombe, Waziri Kindamba amewataka wadau kuwekeza katika sekta ya Utalii kutokana na mkoa huo kuwa na vivutio vingi Ikiwemo hifadhi ya Kitulo na Kipengere.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments