Dkt. Tulia Aipongeza Benki Ya CRDB Kuuenzi Mwezi Ramadhan

 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akipokea zawadi ya mfungo wa mwezi Ramadhani kutoka Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile ikiwa ni sehemu ya utamaduni wa Benki ya CRDB kushirikiana na wateja na makundi mbalimbali ya jamii katika mwezi wa Ramadhani. Dodoma 20 Aprili 2022 –Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dkt. Tulia Ackson. 

Spika ameipongeza Benki ya CRDB kuuenzi mwezi Ramadhani kwa kuwa karibu na jamii katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani. Spika ametoa pongezi hizo akipokea zawadi za mwezi wa Ramadhani kwa niaba ya wabunge ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Benki ya CRDB kushirikiana na wateja wake na makundi mbalimbali katika jamii katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Zawadi hizo zilikabidhiwa katika Ofisi za Bunge na Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile.  Akizungumza wakati wa kupokea zawadi hizo Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson alisema kuwa Benki ya CRDB imekua mstari wa mbele kushirikiana na wadau na kuwataka kuendeleza utamaduni huo hata baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. “Nawapongeza sana Benki ya CRDB kwa kuendeleza utaratibu wao wa kuwa karibu na jamii katika kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani na hasa kwa kugusa makundi mbalimbali hususani wahitaji na niwaombe waendeleze utaratibu huu hata baada ya mwezi Ramadhani” alisema Mh. Tulia  

 Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Undeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile alisema Benki ya CRDB ni benki ya kizalendo inayotambua na kuyaishi maisha ya Mtanzania halisi ambapo kipindi hiki cha Ramadhani ni utamaduni wa Watanzania katika kujumuika pamoja kwa ajili ya ibada na futari. “Pamoja na kuwa leo tupo hapa kwa ajili ya waheshimiwa wabunge lakini tumeendeleza utaratibu wetu wa kufuturisha wateja wetu na makundi yenye mahitaji maalumu ambapo tangu tumeanza mwezi Ramadhani tayari tumeshafanya hivyo kwa mikoa ya Tanga na Shinyanga na wiki hii tunarajia kufanya hivyo kwa mikoa ya Mtwara, Njombe, Mwanza na pia tutafanya hivyo visiwani Zanzibar” aliongeza Bruce. Pamoja na ushiriki katika mfungo wa mwezi Ramadhan kupitia futari na misaada kwa wenye uhitaji, hivi karibuni Benki ya CRDB imeanzisha huduma maalum za fedha inayozingatia misingi ya kutotoa na kupokea riba inayoitwa Al Barakah. Hadi sasa huduma ya Al Barakah imevutia wateja zaidi ya elfu nane huku mikopo iliyotolewa kupitia huduma hiyo ikiwa na thamani zaidi ya Shilingi Bilioni 8. 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments