HAKUNA CHAMA CHA MTU LAZIMA TUSIMAMIE HAKI- KINANA

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wamepiga kura ya kumuidhinisha Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho


Hayo yamefanyika kwenye Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Leo April 01, 2022 Jijini Dodoma ambapo Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Abdulrahman Kinana ameshinda kiti hicho kwa Kura zote 1875 zilizopigwa na Wajumbe ambazo ni sawa na Asilimia 100%

Akizungumza baada ya kushinda Abdulrahman Kinana alimshukuru Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Samia Suluhu Hassan

“Juzi uliniita nikawa najiuliza nimeitiwa nini, nikajua ni katika kusalimiana.Rais akaniambia nataka uwe Makamu Mwenyekiti, nikamwambia sina hiari, sina budi kukubali, napenda kukuhakikishia Mwenyekiti nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kufikia matarajio yako, Niseme sitokuangusha”

Kinana aliishukuru Kamati Kuu kwa kupitisha jina lake, pamoja na wajumbe wa Halmashauri kuu kwa kupitisha na kuidhinisha jina lake

“Mmenipa imani kubwa, na mimi nitakitumikia Chama changu, wana CCM na Watanzania”

Alimshukuru Mzee Mangula ambapo alisema amejifunza mengi kutoka kwake na kumpongeza kwa kustafu kwa Heshima

“Kama Mangula asingeamua kustaafu, basi leo nisingekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi”

Makamu Mwenyekiti Kinana aliwashukuru Wenyekiti wote kuanzia Baba wa Taifa mpaka sasa Rais Samia Suluhu Hassan na kusema kuwa mengine ni mapungufu yake mwenyewe

Aliahidi kwenda kusimamia Chama kuwa imara Kidemokrasia na kusimamia haki ya kuchaguliwa bila upendeleo

Alisema haki nyingine ni kutoa Mawazo

“Lazima wanachama wawe Huru kutoa mawazo, hakuna mwenye hakimiliki ya mawazo, lazima tumsikilize kila mwananchi, na wanachama wakimchagua mtu kwani sisi ni nani wa kupinga”

Alisisitiza kusimamia Demokrasia na kusema ni lazima kusimamia haki

“Nimekuwa nikimsikia Rais akisisitiza mara zote katika kusimamia haki, nilimsikia akisema Vyeti peke yake siyo sifa, Vyeti viende na uadilifu, kukubalika, Nchi hii inajulikana kwa Haki ndani na nje ya Nchi”

Alisema jukumu lake la Tatu ni kwamba CCM si mali ya Serikali ila Serikali zinatokana na CCM ambapo alieleza kuwa CCM haipokei maelekezo kutoka Serikalini

“CCM haiagizwi na Serikali, CCM Inaagiza Serikali, na wanaokwenda kuomba kura ni CCM sio Serikali, niwasihi Viongozi wetu msitudhulumu hiyo haki”

Alisema Serikali inapokuwa na mapungufu wenye jukumu la kuzisemea kasoro ni Chama

“Na hatutazisemea kwa kukejeli, tutaitana kwenye Vikao vyetu vya Ndani, si sawa kwa Mwana CCM kwenda hadharani kuisema vibaya Serikali yake”

Kinana alisisitiza, Chama cha Mapinduzi ni kikubwa na kinakubalika hivyo ni lazima CCM ibaki kuwa masikio kwa Wananchi

Aliahidi utumishi uliotukuka ili Chama kuendelea kuwa imara na umoja

“Hili nalo ni la umhimu, nataka niwasishi hakuna chama cha mtu, kuna Chama cha Mapinduzi.ndani ya hiki chama hakuna ukanda, haya mambo ya ukanda, ukabila, udini tukae nayo mbali.mtu akikosa hoja, maarifa anaingia kwenye kichaka cha udini, ukabila, ubara na visiwani.hiyo si sawa kwa chama hiki, tunaweza kutofautiana kwa sababu nyingi lakini siyo kikanda au kikabila



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments