HUU NI MWAKA WA SENSA, WOTE TUHAKIKISHE TUNAHESABIWA-SHAKA

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka ametoa rai kwa Wananchi wote kushiriki kikamilifu Sensa ya Watu na Makazi inayotarajia kufanyika Agosti mwaka huu.


Akizungumza mbele ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Abdulrhaman Kinana ambaye yuko kwenye ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro, Shaka amesema Sensa ni muhimu kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo.

“Mwaka huu ni mwaka wa Sense ya Watu na makazi, hivyo tunao wajibu wa kuhamasishana kushiriki katika sensa na kila mtu ahakikishe anahesabiwa, sensa ina faida kubwa kwa CCM ambayo ndio imeunda Serikali kwani itajua namna ya kuwatumikia wananchi kwa kuwa na idadi kamili ya watu.

“Hamuwezi kuwa na mipango ya Serikali ambayo itakuwa ya kubahatisha, ili tuwe na mipango inayotekelezeka lazima tujuane na sensa ndio itafanya tujuane tuko wangapi.Sensa ambayo inatumika sasa ilifanyika mwaka 2012 , hivyo huenda hata fedha zinazokuja hapa Kilimanjaro ni ndogo ukilinganisha na watu waliko,”amesema Shaka.

Amefafanua viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro wamesoma taarifa ya fedha ambazo zimetolewa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia kwa ajili ya maendeleo, lakini kukiwa na sensa huenda fedha zikaongezwa kulingana na watu walioko kwa sasa.

Katika hatu nyingine Shaka akizungumza mbele ya Kinana na wanachama wa CCM waliojitokeza kwa wingi kwenye kikao kazi cha ndani, amewakumbusha wanachama wa Chama hicho kuhakikisha hawafanyi makosa katika chaguzi zijazo kwani moja ya malengo ya CCM ni kuendelea kushika dola.

“Hatuna sababu ya kufanya makosa tunakwenda kwenye uchaguzi wa ndani na mwaka 2025 tutakuwa na Uchaguzi Mkuu, hivyo Mkoa wa Kilimanjaro hakikisheni mnaendelea kushika dola.

“Taarifa ya Mkoa wa Kilimanjaro imeeleza kwa kina mafanikio lukuki yaliyopatikana chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia.Kilimanjaro itaendelea kubadilika kutokana na uthubutu wake wa kusimamia maendeleo.

“Mungu ametupa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anajua watanzania wanataka nini katika kufikia maendeleo ya Taifa letu.Mungu ametupatia Makamu Mwenyekiti wa CCM anayejua namna ya kumshauri Mwenyekiti wetu na Rais katika kuhakikisha tunaendelea kupiga hatua kimaendeleo.”

Aidha Shaka amewaomba CCM kuendelea kuimarisha umoja na mshikamano na msingi wa Chama hicho umewekwa kwenye umoja na mshikamano, na umoja wao ndio ushindi wao na ili watafsiri kwa kwa vitendo maelekezo ya Chama ushindi ni lazima.

“Ni vema umoja na mshikamano ukaimarishwa, hivyo nitoe rai kwa viongozi wa ngazi mbalimbali kukisemea chama chetu kwa yale yaliyofanywa, tunafahamu huku kwenye Chama kazi yetu ni kulinda dola na dola tutailinda kwa kufanya mambo ya msingi kwa ajili ya wananchi.

“Na tumeingia mkataba kati yetu na serikali.Hata hivyo hapa Kilimanjaro kuna propaganda zinasema huduma ya usafiri wa treni imesimama katika serikali ya Awamu ya Sita jambo ambalo si kweli.

“Hivyo viongozi wanatakiwa kusema ukweli kuwa hizo ni propaganda ambazo hazina tija. Ilani ya CCM ilishatoa maelekezo ya kuimarishwa kwa huduma ya usafiri wa treni, hivyo nataka kuwambia Serikali ya Rais Samia itaendelea kuimarisha usafiri wa treni.”amesema.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka akizungumza mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana pamoja na wanachama wengine wa Chama hicho mkoa wa Kilimanjaro wakati wa kikao cha ndani kilichowakutanisha wanaCCM kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo leo Aprili 26,2022
Wanachama wa CCM wakiwa wamesimama kuimba moja ya wimbo wa Chama hicho walipokuwa wakimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana .
Wakuu wa Wilaya kutoka mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini wakati mkutano ukiendelea
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka akishiriki kucheza ngoma iliyokuwa inaimbwa na kundi la Msanja kutoka Njoro  mkoani Kilimanjaro
Sehemu ya mabalozi wa CCM wakisikiliza yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mkutano huo wa Kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Kilimanjaro leo Aprili 26,2022.
 Na Said Mwishehe.Kilimanjaro

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments