Iran Yatafakari Kuwapokea Wageni Wa Kombe la Dunia la Qatar

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imewasilisha pendekezo la kuwaruhusu raia wa kigeni watakaofika Qatar kama watazamaji wa Kombe la Dunia la FIFA 2022 kuingia Iran bila kulipia visa.

Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Iran (IRNA), mpango huo utajumuisha raia wote wa kigeni watakaotembelea Qatar kwa ajili ya Komble la Dunia la 2022 isipokuwa raia wa Uingereza, Marekani, Canada na pia Pakistan, Afghanistan, India, Bangladesh, Somalia na Sri Lanka.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa wageni hao watapata visa ya miezi miwili na pia wanaweza kupata idhini ya kuingia na kutoka Iran mara kadhaa.

Aidha kwa mujibu wa pendekezo hilo, raia wa nchi ambazo zimefuzu kuingia katika Kombe la Dunia la Qatar la 2022, watapata visa ya kuingia Iran bila malipo na pia hawatahitajika kuwasilisha nyaraka zozote.

Tangazo hilo limekuja huku Iran ikiwa inatekeleza mkakati maalumu wa kutumia fursa ya Kombe la Dunia katika nchi jirani ya Qatar kuimarisha utalii nchini.

Iran imetangaza mpango wa kuisaidia Qatar kufanikisha Kombe la Dunia ambalo litafanyika kuanzia Novemba 21 hadi Disemba 18 mwaka huu.

Waziri wa Barabara na Mawasiliano wa Iran Rostam Qassemi na mwenzake wa Qatar Jassim bin Saif Al Sulaiti wanatazamiwa kukutana leo na kesho katika kisiwa cha Kish kusini mwa Iran ili kujadili namna kisiwa hicho kinavyoweza kutumiwa kama makazi ya timu na mashabiki wa Kombe la Dunia.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments