KASI ZAIDI OPERESHENI YA UANDIKISHAJI WA ANUANI ZA MAKAZI NA POST CODE IKUNGI IMEFIKIA ASILIMIA 90

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro pamoja na wajumbe wa kamati ya usalama wameendelea na zoezi la uhamasishaji, utoaji wa elimu na ukaguzi wa operesheni ya uandikishaji wa anuani za makazi na post code katika tarafa ya ikungi

Wakiwa katika kata ya Isuna kijiji cha nkuhi, na kata ya mkiwa walishuhudia zoezi la uandikishaji wa anuani za makazi likiendelea kwa kasi uku wakipata nafasi ya kujibu maswali mbalimbali ya viongozi na wanachi na kutoa elimu ya namna bora ya kuendelea na zoezi hilo katika vijiji na vitongoji vyote vya kata ya isuna na mkiwa


Mpaka sasa wilaya ya Ikungi imefikia asilimia 90 ambapo zaidi ya makazi elfu hamsini-(50,000) yameshaandikishwa kati ya matarajio ya uandikishaji wa makazi elfu hamsini na tano-55,000 kwa wilaya ya ikungi.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments