Katibu Mkuu CUF aeleza matamanio yake kukirejesha chama mstarini


Siku chache baada ya kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Hamad Masoud Hamad amesema anatamani kuona chama hicho kikirejesha nguvu iliyokuwa nayo awali.

Hamad aliyechaguliwa kushika nafasi hiyo Machi 25, 2022 ametoa kauli hiyo leo alipopokewa Zanzibar na kukabidhiwa ofisi makao makuu ya chama hicho Mtendeni, Mjini Unguja.

Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa chama hicho na waandishi wa habari, Hamad amesema  atatumia uzoefu wake kurejesha misingi yote ya chama hicho.

“Hakuna asiyejua kwamba CUF kilikuwa chama kikubwa hapa nchini lakini kwa sasa kimetetereka sasa tunaenda kukisuka upya kirejee katika hali yake ya zamani,” amesema

Amesema chama hicho kilifikia hatua ya kuwa na wabunge wengi ndani ya bunge la Tanzania na wawakilishi katika baraza la wawakilishi Zanzibar na kukiwezesha kupata ruzuku ya mamilioni ya fedha lakini hayo yote yamepotea.

“Haya sasa ndio tunataka kuyarejesha kwahiyo tunatuma salamu kwa vyama vingine vijiandae na tunawahakikishia tutafikia huko katika uchaguzi wa mwaka 2025," amesema

Amesema kazi yake ya kwanza ndani ya chama akiwa mtendaji mkuu wa chama ni kusimamia uchaguzi wa chama hicho unaotarajia kufanyika kuanzia Mei hadi Oktoba mwaka huu

Mbali na kusimamia masuala ya utendaji ndani ya CUF, Hamad amesema atahakikisha anasimamia mali za chama hicho ili ziweze kukaa katika mstari wake.

Masoud Hamad aliyekuwa mwanachama na mgombea nafasi ya Uenyekiti Taifa katika chama cha ACT Wazalendo alirejea CUF Februari, 2022

Februari 8, Hamad Masoud aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya ACT Wazalendo alitangaza rasmi kujiondoa ndani ya chama hicho kwa kile alichodai kufanyiwa udhalilishaji katika kipindi cha uchaguzi wa ndani wa chama hicho uliofanyika Janauri 29 na Juma Duni Haji kuibuka mshindi.

 Unguja. 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments