Mkurugenzi wa Idara ya Sheria Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Michael Luena akizungumza katika kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022.
Sehemu ya Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya wakiwa katika kikao kazi na mafunzo cha wenyeviti hao kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi Benhaji Masoud akiwasilisha mada kwenye kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022.
Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini Stella Tullo akizungumza wakati wa kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Zakariyya Kerra akizungumza katika kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022.
Sehemu ya Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya wakiwa kwenye kikao Kazi na Mafunzo cha Wenyeviti hao kinachoendelea mkoani Tanga tarehe 4 April 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
Kikao Kazi na Mafunzo kwa Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya nchini kimeanza leo tarehe 4 April 2022 mkoani Tanga.
Kikao hicho kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete.
Katika kikao hicho pamoja na uwasilishwaji mada, Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya nchini watapata mafunzo ya namna bora ya kuendesha mashauri ya ardhi pamoja na uandishi mzuri wa hukumu.
Katika siku ya kwanza ya kikao hicho Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi Benhaji Masoud aliwasilisha mada kuhusiana na masuala mtambuka katika uendeshaji mashauri ya ardhi.
Kikao hicho cha siku nne kinatarajiwa kumalizika siku ya alhamisi tarehe 7 April 2022.
Na Mwandishi Wetu, TANGA
0 Comments