KMC YAREJEA UWANJA WA UHURU, KUIKABILI NAMUNGO KESHO

KIKOSI cha KMC FC leo kimefanya maandalizi yake ya mwisho kuelekea katika mchezo wake wa Ligi kuu ya NBC Soka Tanzania Bara dhidi ya Namungo ya Ruangwa Mkoani Lindi utakaopigwa hapo kesho katika Uwanja wa Uhuru hapa jijini Dar es Salaam saa 16:00 jioni.

Kwa mujibu wa barua iliyotumwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania TPLB, ilieleza kwamba mchezo huo utapigwa siku ya MAJIya Aprili tatu mwaka huu katika uwanja huo wa Uhuru badala ya Azam Complex Chamanzi kama ratiba ya awali ilivyoelekeza kutokana na kukamilika kwa matengenezo yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja huo.

Kutokana na barua hiyo ya TPLB, Timu ya Manispaa ya Kinondoni inarejea sasa katika uwanja wake wa nyumbani ikiwa ni baada ya kupita kwa takribani michezo mitano ikicheza nje ya uwanja huo na hivyo kulazimika kutumia uwanja wa Azam Complex Chamanzi ambapo mara ya mwisho kutumia uwanja huo wa Uhuru ilikuwa ni kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Azam FC na KMC kupata ushindi wa magoli mawili kwa moja.

KMC FC chini ya Kocha Mkuu Thierry Hitimana hadi sasa imejiandaa vema kweye mchezo huo licha ya kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kwamba Timu ya Namungo imekuwa ikifanya vizuri katika michezo yake lakini ubora wa wachezaji pamoja na Benchi zima la ufundi litahakikisha kuwa alama tatu muhimu zinapatikana.

“Tumetoka kupoteza michezo miwili mfululizo, na tunakwenda kwenye mchezo mwingine tukiwa nyumbani, hii ninafasi kwetu ya kusahihisha makosa ya awali na kwamba Kocha Mkuu Hitimana katika kipindi hiki ambacho Timu zilikuwa kwenye mapumziko kupisha kalenda ya FIFA amefanya maboresho kwenye maeneo ambayo aliona yanachangamoto ambazo zilikosesha Timu kupata matokeo mazuri, hivyo mashabiki zetu watarajie kupata burudani.

Kwakipindi kirefu hatujatumia uwanja wetu halisi wa nyumbani, na sasa tunarejea kwenye mchezo dhidi ya Namungo, hivyo Tunaipongeza TPLB kwa ushirikiano mkubwa waliotuonesha kwa kipindi chote hicho na sasa tunakwenda kesho tukifahamu kabisa mchezo utakuwa mgumu lakini KMC FC tumejipanga kuondoka na alama tatu muhimu.

Aidha Klabu ya KMC FC inawasihi mashabiki kujitokeza kwa wingi siku ya kesho kwenye mchezo huo muhimu ambao wachezaji wamejiandaa vizuri kuhakikisha kwamba wanatoa burudani iliyoambatana na ushindi, ukizingatia kuwa itakuwa siku ya wekeand.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments