MAADHIMISHO YA 58 YA MUUNGANO SINGIDA YATUMIKA KUWAFUNDA VIJANA.

Vijana mkoani Singida wametakiwa kujiamini, kuonesha na kuvitumia vipaji walivyonavyo katika kuleta ubunifu na ugunduzi wa mambo kwa kuwa wengi wana vipaji lakini hawajavitambua.

Akiongea katika Kongamano la maadhimisho ya 58 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha uhasibu (NlT) uliyopo mkoani hapo kwa kuwashirikisha Vijana wa Mkoa wa Singida katika makundi mbalimbali,Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro amewataka vijana kuhakikisha wanatumia akili zaidi kuliko elimu katika kutambua vipaji walivyonavyo na kuchukua hatua.

Akieleza umuhimu wa vijana kutumia akili zaidi kuliko elimu DC Muro amesema kwamba duniani wagunduzi wakubwa hawakutumia elimu lakini walitumia akili na wakafika mbali hivyo kuwataka wajitume na waweze kutumia vipaji vyao kama njia ya kupitisha elimu wanazopata.

Aidha Mkuu wa Wilaya Muro amebainisha kwamba kijana anayemaliza chuo na kukaa mtaani akisubiri Serikali itoe ajira ni matokeo mabaya ya matumizi ya vipaji kwa kuwa kila mmoja amepewa kipaji chake.
                      
Amewataka vijana kujiunga katika vikundi na kuvisajili ili waweze kupata mikopo kupitia asilimia Nne katika Halmashauri zao huku akiwakumbusha Maafisa Maendeleo ya Jamii kuendelea kutoa msaada wa mawazo kwa vijana wenye vikundi.

Muro ameendelea kusema kwamba huenda matumizi mabaya ya simu janja ndio chanzo cha vijana kushindwa kufikiria vizuri namna ya kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo ugunduzi wa vipaji vyao na namna ya kupata mitaji na utajiri kwa ujumla.

Amewataka vijana kutumia Kongamano kuzitumia fursa ambazo zimekuwa zikioneshwa katika mada mbalimbali zilizowasilishwa, na kila mwenye kipaji kuanza kuzitumia.

                             
Kwa upande wake Afisa Vijana Mkoa wa Singida na mratibu wa Kongamano hilo Frederick Ndahani amesema lengo la Kongamano hilo ni kuonesha fursa za kiuchumi ambazo zimezunguka Mkoa wa Singida ili waweze kuzitumia na kujikwamua katika maisha yao ya kila siku.

Aidha akieleza jitihada za Serikali katika Mkoa wa Singida zakuwainua vijana amesema katika kipindi cha mwaka 2018/2022 Mkoa umetoa jumla ya Tsh. Milioni 601.4 ikiwa ni mikopo iliyotolewa katika viku





 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments