MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MWENGE MKOANI NJOMBE YA PAMBA MOTO

 

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi akifanya ukaguzi wa Maandalizi ya Uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe tarehe 31 Machi, 2022, (kulia kwake) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Njombe wakifuatilia vijana wa halaiki wakiwa wanafanya mazoezi ya mandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe 

 

Vijana wa halaiki wakiwa wanafanya mazoezi ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe tarehe 31 Machi, 2022, Mbio hizo zitazinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Isdor Mpango

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Jamal Katundu pamoja na  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo – Zanzibar, Bi. Fatma Rajabu wakifuatilia ukaguzi wa maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe 

Vijana sita walioandaliwa kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, watakaokabidhiwa jukumu la kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Mikoa 31 na Halmashauri 195 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa siku 195, wakiwa katika maandalizi ya Uzinduzi wa mbio hizo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana, (katikati) akifuatilia maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa Njombe, Waziri Kindamba na kushoto kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas katambi, wengine ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Jamal Katundu pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Bi. Fatma Rajabu.

Mkurugenzi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Idara ya Maendeleo ya Vijana, Bw. Julius Tweneshe akitoa ufafanuzi juu ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe, tarehe 02 Aprili, 2022.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments