Majaliwa Aagiza Wizara, Taasisi Kuimarisha Vitengo Vya Ufuatiliaji na Tathmini

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza wizara na taasisi ziimarishe vitengo vya kufanya ufuatiliaji na tathimini kwa ajili ya kupata ufanisi na mrejesho stahiki wa utekelezaji wa majukumu ya miradi mbalimbali.

Majaliwa ameto agizo hilo leo Jumatano Aprili 27,2022 wakati akifungua kongamano la kwanza la kitaifa la wiki ya ufuatiliaji na tathimini liloandaliwa na Umoja wa Tathimini Nchini (Tanea) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

 “Taasisi zote za umma zihakikishe zinaandaa mipango ya ufuatiliaji na tathimini ya mwaka mmoja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mwongozo ufuatiliaji na tathimini ya miradi programu za maendeleo ambazo pia nitahitaji kuziona kutoka katika wizara,”amesema.

Amesema ni matarajio ya Serikali kuwa mfumo wa ufuatiliaji na tathimini utawaondoa katika fikra nadharia ya ufuatiliaji na tathimini na kwenda katika vitendo vya uhalisia ambavyo pia vitatoa matokeo.

Majaliwa amesema ni vyema kama nchi kuwa na mfumo wa ufuatiliaji na tathimini na kuwapongeza Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuanzisha kitengo hicho cha Tanea na kuwataka kuendelea kupanua wigo.

Hata hivyo, amesema bado kuna changamoto ya udhaifu katika matumizi sahihi ya taarifa wanazozipata baada ya kufanya tathimini ambayo inatokana kutojipanga vizuri.

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amesema kwasasa ofisi yake imeanza kubaini na kukusanya mifumo na data na kuioanisha ili kuwa na taarifa sahihi na kwa wakati ambazo zitasaidia katika  kufanya maamuzi ya kisera na kimkakati.

“Vile vile wataalamu wachache wa ufuatiliaji na tathimini katika vitengo mbalimbali vya Serikali na hiyo pia ni changamoto katika kuhakikisha kwamba eneo hili la ufuatiliaji na tathimini linafanya kazi vizuri,”amesema.

Mwenyekiti wa Tanea, Profesa Deus Ngaruko amesema kumekuwa na changamoto kadhaa za ufuatiliaji na tathmini nchini ikiwemo kukosa uhitaji na utumiaji wa taarifa za ufuatiliaji na tathmini kwenye kupanga mipango ya maendeleo

“Kutokuwepo kwa Sera ya ufuatiliaji na tathmini nchini Tanzania na Kutotambulika kwa tasnia ya ufuatiliaji na tathmini kwenye mfumo wa ajira (Scheme of service),” amesema.

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments