MARUFUKU LUMBESA ZAO LA VITUNGUU MKOANI SINGIDA

 

Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili akizungumza na Wakulima na Wafanyabiashara wa Vitunguu wa Soko la Kimataifa lililopo mkoani hapa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Dk.Binilith Mahenge ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo kwa Mkoa wa Singida yameadhimishwa kwa kufanya usafi katika soko hilo.


Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida Ally Mwendo akizungumza katika mkutano huo


Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Kulanga Kanyanga akitoa shukurani baada ya shughuli ya usafi kufanyika kwenye soko hilo.


Naibu Meya wa Manispaa ya Singida, Hassan Mkata akichangia jambo wakati wa mkutano huo.

Kaimu Katibu Tawala Manispaa ya Singida Ally Mwendo akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili wakati wa mkutano huo.

Mwenyekiti wa soko la Kimataifa la Vitunguu, Mkoa wa Singida, Iddi Mwanja akizungumza kwenye mkutano huo.
Usafi katika soko hilo la vitunguu ukifanyika.
Wafanyabiashara wa soko hilo wakiendelea na usafi.
Usafi ukifanyika.
Kazi ya usafi ikifanyika.
Wanafunzi wakishiriki kufanya usafi katika soko hilo.
Takataka zikipakiwa katika gari baada ya kuondolewa kwenye soko hilo.
Usafi ukifanyika.
Naibu Meya wa Manispaa ya Singida, Hassan Mkata, akishiriki kufanya usafi katika soko hilo.
Gari likisomba takataka wakati wa zoezi hilo.
Usafi ukifanyika kwa mavazi maalumu ili kujilinda na magonjwa yatokayo na uchafu.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Vitunguu vikiuzwa katika soko hilo.
Vitunguu vikiwa kwenye magunia yenye uzito wa kilo 100 unaokubalika badala ya lumbesa.

MKUU wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge amepiga marufuku wafanyabiashara kununua mazao ya wakulima kwa kutumia vipimo ambavyo havikubaliki lumbesa ambavyo vinatumika kuwaibia wakulima.

Marufuku hiyo imetolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili wakati akizungumza na wakulima na wafanyabiashara wa vitunguu wa soko la kimataifa lililopo mkoani hapa katika maadhimisho ya Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo kwa Mkoa wa Singida yameadhimishwa kwa kufanya usafi katika soko hilo.

"Serikali ilikwisha piga marufuku mfumo huo wa lumbesa na tutaendelea kulisimamia jambo hilo na kwa mfanyabiashara atakaye bainika anafanya hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake" alisema Muragili.

Alisema matumizi ya lumbeza  yamekuwa yakiwaumiza wakulima wa zao la vitunguu ambavyo vinalimwa kwa wingi mkoani Singida.

Muragili alisema kipimo kinachokubalika ni mizani na gunia lenye mazao la ujazo wa kilo 100 na si zaidi ya hapo na kuwa matumizi ya vipimo vingine ambavyo si rasmi  ni ulanguzi jambo ambalo halikubaliki hata kidogo.

Akizungumzia zoezi za ufasi aliwataka wananchi wa Mkoa wa Singida kuzingatia usafi wakati wote ili mkoa huo uwe namba moja hapa nchini kwa usafi.

"Suala la usafi sasa liwe la kila siku na endelevu katika maeneo yote ya mkoa wetu lengo letu ni kuifanya Singida kuwa bora katika utunzaji wa mazingira na usafi kwa ujumla" alisema Muragili.

Katika hatua nyingine Muragili alimtaka mkandarasi anayefanya usafi katika soko hilo  kuhakikisha magari ya kusomba takataka  yanakuwepo katika eneo hilo wakati wote na akamtaka kuanzia leo kuondoa takataka zote zilizopo ili kuwaondolea adha wafanyabiashara kufanya kazi zao kwenye eneo ambalo ni chafu.

Aidha Muragili alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi litakapo wadia na zoezi la kitafifa la njano ya polio kwa watoto waliochini ya miaka mitano ambalo linafanyika nchi nzima.

Mwenyekiti wa Soko la Kimataifa la Vitunguu la Mkoa wa Singiida Iddi Mwanja alimuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuangalia  kwa karibu suala la lumbesa kwa wakulima nchini hasa wa vitunguu kutokana na wizi mkubwa wanaofanya wafanyabiasha hao wasio waaminifu.

Alisema hali imekuwa mbaya zaidi katika Mkoa wa Iringa ambapo rushwa imekuwa ikitumika kupitisha magunia ya bidhaa hiyo yenye ujazo wa zaidi ya kilo 100 hivyo kuharibu soko la zao hilo katika maeneo mengine ya nchi.
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments