MIGODI YA BARRICK YATOA MSAADA WA VIPIMO VYA MAGONJWA YA KISASA

 

Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara , Apolinary Lyambiko, akimkabidhi mashine za vipimo kwa viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Mara.
Viongozi wa Chama na Serikali mkoani Mara katika picha ya pamoja na Maofisa wa Barrick katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Ally Happi, akiongea katika hafla ya kupokea vifaa vya vipimo (Kushoto) ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara , Apolinary Lyambiko
Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Apolinary Lyambiko, akiongea katika hafla ya kukabidhi mashine za kisasa za kupima magonjwa.
Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO) wa Mara, Dkt Juma Mfanga akiongea wakati wa hafla hiyo.
Wageni waalikwa katika hafla hiyo wakifuatilia matukio.


Migodi ya Barrick ya North Mara na Bulyanhulu imetoa msaada wa vipimo vya kisasa vya utambuzi wa magonjwa katika hospitali mbili za mikoa kama sehemu ya mpango wa kusaidia nchi katika kupambana na kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.

Katika hafla ya kukabidhi msaada huo katika Hospitali ya Rufaa ya Musoma, Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara , Apolinary Lyambiko, alikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Ally Happi, vifaa vya kisasa vya kupima magonjwa ya kuambukiza kama virusi vya UVIKO-19, Kifua Kikuu, Nimonia, Mafua makali na magonjwa mengineyo.

Daktari Mkazi katika mgodi wa North Mara, Dk. Nicholas Mboya, alibainisha kuwa utambuzi unaweza kufanywa kupitia aina mbalimbali za sampuli, kwa kuchukua vipimo kwenye pua, Koo, mate au makohozi, na kutoa majibu kati ya muda wa dakika 49 na 80. 

Alisema Upimaji huu unadhihirisha ubora wa vipimo hivi vya kisasa ambavyo vinaweza kutambua majibu ya sampuli nne kwa wakati mmoja.

"Tunajivunia kutoa vifaa hivi maalum ili kuimarisha miundombinu ya matibabu katika jamii zinazozunguka migodi ya kampuni," Lyambiko", alisema.
Chanzo Na Malunde 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments