Recent-Post

MKUTANO MAALUM WA 47 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA EAC NGAZI YA WATAALAM UMEFUNGULIWA JIJINI ARUSHA

 Mkutano Maalum wa 47 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki unafanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 4 hadi 6 Aprili 2022.


Mkutano huu unafanyika katika mpangilio ufuatao; tarehe 4 Aprili 2022 Mkutano Ngazi ya Wataalam, tarehe 5 Aprili 2022 Mkutano Ngazi ya Makatibu Wakuu na tarehe 6 Aprili 2022 Mkutano Ngazi ya Mawaziri.

Pamoja na mambo mengine Mkutano Ngazi ya Wataalamu unaandaa taarifa ya masuala ya Fedha na Utawala itakayowasilishwa kwenye mkutano wa Makatibu Wakuu na baadae kwenye mkutano wa Mawaziri.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Justin Kisoka (kushoto) akichangia hoja katika Mkutano Maalum wa 47 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Ngazi ya Wataalam unaofanyika leo tarehe 4 Aprili 2022 jijini Arusha, Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Bw. Eliabi Chodota akifatilia mkutano huo.

Mkutano ukiendelea, kulia ni ujumbe wa Tanzania ukifuatilia majadiliano katika mkutano huo.
Meza kuu ikiongoza Mkutano.
Mkurugenzi Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Caroline Chipeta akifatilia majadiliano katika mkutano.
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania
Ujumbe kutoka taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ukifuatilia majadiliano.

Post a Comment

0 Comments