Recent-Post

Ofisi Ya Rais Inavyomulikwa Kwa Utawala Bora, Utumishi

Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora ni miongoni mwa wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais zikiratibu masuala mtambuka ya utawala na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Ofisi hiyo imegawanyika katika Ofisi ya Rais Ikulu, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Taasisi ya Uongozi, Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania (Mkurabita), Wakala wa Ndege za Serikali na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).

Miongoni mwa majukumu yake ni kuratibu majukumu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano katika masuala ya Siasa, Uchumi, Jamii, Sheria, Diplomasia, Mawasiliano na Habari, Uhusiano wa Kikanda, Kimataifa na ushauri mwingine kwa lengo la kumsaidia Rais kufanya maamuzi.

Katika mwaka wa fedha 2021/22 Wizara ilitengewa zaidi ya Sh727.93 bilioni, matumizi ya kawaida ni zaidi ya Sh544.57 bilioni na miradi ya maendeleo Sh183.35 bilioni.

Miongoni mwa mafanikio katika wizara hiyo wa kipindi cha mwaka mmoja ni hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kukutana na vyama vya siasa kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Pia, kumekuwa na kikosi kazi kilichoundwa kwa lengo la kuratibu maoni ya vyama vya siasa.

Mafanikio mengine ni kuimarishwa kwa uhusiano wa kimataifa na diplomasia.

Pia, Rais Samia amefanya ziara za kimataifa akihamasisha uwekezaji, ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

 

Post a Comment

0 Comments