Rais Samia Aeleza Sababu Kufanya Mabadiliko Madogo Baraza la Mawaziri

Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza sababu ya kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyohusisha uhamisho wa mawaziri watatu.

Machi 31, 2022 Rais Samia alifanya mabadiliko ambapo aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene alihamishwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera na Uratibu huku nafasi yake ikichukuliwa na Damas Ndumbaro.

Waziri Ndumbaro yeye alihamishwa kutoka Wizara ya Maliasili na utalii nafasi ambayo sasa imechukuliwa na Pindi Chana ambaye kabla ya hapo alikuwa Waziri wa Bunge, Sera na Uratibu.

Akizungumza leo Jumamosi Aprili 2, 2022 Rais Samia amesema mabadiliko yaliyofanyika kwa mawaziri ni marekebisho kwa kuwa wote bado wanasomana.

Amesema Serikali imedhamiria kukuza uchumi baada ya kupigwa na Uviko 19 na katika kukuza uchumi lazima wote wafanye kazi kwa bidii na kila mtu katika sekta anayosimamia kuzungumza lugha moja.

 “George kwa uzoefu wako na ulishakaa sana Bungeni, na ni bingwa wa sheria nikaona uende pale kwa Waziri Mkuu ukamsaidie kusimamia Bunge, Sera. Kwa uzoefu wako unaweza kumsaidia Waziri Mkuu kuratibu wenzako” amesema Rais Samia.

“Damas nimeona uende kwenye hiyo Wizara ukasimamie sheria zetu, marekebisho pale panapolega ukakaze nati, Pindi kwa sifa zilizosemwa hapa kubwa zaidi nadhani wewe ni mwanasheria lakini kwa kuwa ulishapita kwenye Diplomasia na Menejimenti ya Maliasili na Utalii nimeona utakaa vizuri zaidi”

Rais Samia awaapisha mawaziri

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments