Rais Samia: Utaifa Utangulizwe Majadiliano TCD

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wajumbe wa mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), unaojadili maridhiano, haki na amani kuweka mbele utaifa na wazingatie mazingira yaliyopo hapa nchini.

Rais Samia ameeleza hayo leo Jumanne Aprili 5, 2022 Jijini Dodoma wakati akizindua mkutano huo wenye lengo la kujadilili maeneo matatu ya mardhiano, haki na amani.

Mkutano huo wa siku mbili utahusisha kumkabidhi uenyekiti wa TCD, Abdulrhaman Kinana baada ya Zitto Kabwe kumaliza muda wake.

“Nilikuwa naangalia alipokaa Kinana hadi mstari wa mwisho wote ni Watanzania isipokuwa wenzetu wachache ni wageni. Sisi ndio tunaoguswa na mkutano huu, tunayoyazungumzwa yazungumzwe Kitanzania. 

“Tunapozungumza maridhiano, tunayazungumza vipi au tunaridhiana wapi? Katika maeneo yapi na tunakwenda hadi wapi? Au Haki zetu ni zipi Watanzania haki zetu ni zipi kama vyama vya siasa. Tutazungumza haki zetu na pale ilipobinywa tuzungumze namna ya kuifungua lakini kwa mazingira ya Utanzania.

 Amesema baada ya hapo wanakwenda kudumisha amani, lakini akatoa angalizo ya kwamba hakuna atakayewasaidia katika mchakato huo isipokuwa Watanzania pekee.

“Hakuna atakeyetusaidia katika hili kwenye hili, hawa watatusaidia kukusanyika na posho lakini haya mambo matatu ya maridhiano, haki na amani ni ya kwetu. Tanzania itabaki kuwa moja na haitagawanyika," amesema Rais Samia.

"Nikiwa mdau wa demokrasia fursa hii ya kukutana hapa ni adhimu kwa ajili ya kujdaliana na kujenga kushaurina ana kujenga mwafaka, umoja na mshikamano wa kitaifa,"


 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments