Saudia Yaruhusu Waislamu Milioni Moja Kutekeleza Ibada ya Hija Mwaka Huu

Utawala wa Saudia umetangaza Jumamosi kwamba nchi hiyo itawaruhusu Waislamu milioni moja kushiriki katika ibada inayokuja ya Hija.

Saudi Arabia ilisema Jumamosi itawaruhusu Waislamu milioni moja kutoka ndani na nje ya nchi kushiriki katika Hija mwaka huu, hii ikiwa ni idadi kubwa zaidi baada ya vizuizi vya janga la corona kulazimisha kupunguzwa idadi ya mahujaji katika kipindi cha miaka miwili mfululizo.

Wizara ya Hija imesema katika taarifa yake kuwa "imeidhinisha mahujaji milioni moja, wa kigeni na wa ndani, kutekeleza ibada ya hija mwaka huu."

Moja ya nguzo tano za Uislamu, Hija inapaswa kutekelezwa na Waislamu wote wenye uwezo angalau mara moja maishani. Hija kwa kawaida huwa  moja ya mikusanyiko mikubwa zaidi ya kidini ulimwenguni, ambapo mwaka 2019 takriban Waislamu milioni 2.5 walishiriki katika ibada hiyo.

Lakini baada ya kuanza kwa janga la coronavirus mnamo 2020, viongozi wa Saudia waliruhusu mahujaji 1,000 tu kushiriki.

Mwaka uliofuata, waliruhusu tu wakaazi wa Saudia kushiriki katika ibada ya Hija ambapo washiriki 60,000 waliochanjwa kikamilifu waliochaguliwa kupitia bahati nasibu

Waumini wakiwa katika ibada ya 

Vizuizi hivyo hivyo vya Hija vilivyowekwa na Saudia vimekosolewa sana na Waislamu walio nje ya nchi ambao walizuiliwa kushiriki ibada ya Hija mwaka jana. Tangazo la Jumamosi lilisema kuwa hija ya mwaka huu itakuwa tu kwa mahujaji walio na chanjo na ambao wana umri wa chini ya miaka 65.

Wale wanaotoka nje ya Saudi Arabia watahitajika kuwasilisha matokeo hasi ya Covid-19 PCR kutokana na kipimo kilichochukuliwa ndani ya saa 72 kabla ya kusafiri.

Serikali inataka kuhakikisha usalama wa mahujaji "huku ikihakikisha kwamba idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani kote wanaweza kutekeleza hija", taarifa ya Jumamosi ilisema.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments