SIMBA SC IYOOOO ROBO FAINALI, YAINYUKA US GENDARMERIE 4-0

 

SIMBA na RSB Berkane zimetinga kibabe hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupata ushindi katika mechi zao za mwisho Kundi D.

Simba akicheza uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam wameichapa US Gendarmerie mabao 4-0 bao la kwanza likifungwa na Sadio Kanoute dakika ya 63.

Mabao mawili yamefungwa na Chris Mugalu dakika ya 68 na 78 huku bao la nne akijifunga mlinda mlango wa US Gendarmerie Saidu Hamisu baada ya mpira kurudishiwa na beki wake.

Berkane nao wameifunga ASEC Mimosas bao 1-0 likipatikana dakika ya 28 likifungwa na Chadrack Lukombe kwa Mkwaju wa Penalti

Kwa ushindi huo Timu hizo zimemaliza zikiwa na Pointi 10 kila mmoja huku RSB Berkane wakiongoza wakiwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa nafasi ya tatu ikishikwa na ASEC Mimosas Pointi 9 na US Gendarmerie wakimaliza wa mwisho kwa pointi zao

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments