SIMBA SC YAPOKEA KICHAPO KWA MIKWAJU YA PENATI 4-3 NA ORLANDO PIRATES


KWA mara nyingine Simba wameshindwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuondoshwa na Orlando Pirates kwa mabao 4-3 kwa Mkwaju wa Penalti.

Hatua hiyo ya Penalti imetokana na wenyeji kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kupelekea timu hizo kwenda hatua ya Matuta baada ya mechi ya Kwanza Simba kushinda bao 1-0 uwanja wa Benjamin Mkapa.

Orlando Pirates wameibuka na ushindi huo baada ya kupata Penalti 4-3 huku Simba wakikosa Penalti mbili wachezaji waliokosa ni Jonas Mkunde na Henock Inonga huku wenyeji wakikosa Moja.

Simba walipata pigo dakika ya 58 Chris Mugalu kuonyeshwa kadi nyekundu mara baada ya kadi hiyo Orlando Pirates walipata bao kupitia kwa Kwame Peprah kufunga bao dakika 60.

Kwa ushindi huo Orlando Pirates wametinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho na watamsubiri mshindi kati ya Al Ahli Tripoli au Al-Ittihad zote kutoka Libya

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments