Sitta Ataka Mwongozo Wa Upelekaji wa Watumishi Vijijini

Mbunge wa Urambo (CCM), Margaret Sitta amesema wafanyakazi wanapelekwa kwenda kufanya kazi vijijini kwa staili ya zamani kwa kuwekwa katika malori.

 Akichangia katika makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) leo Jumanne Aprili 19, 2022, Sitta amesema wafanyakazi wengine hawapajui wanapokwenda.

“Wengine hawajui hata shule ama kituo cha afya hakijui (anapokwenda) wizara (Tamisemi) itoe mwongozo wa jinsi ya kupokea wafanyakazi. Kuwe na mpango maalumu wa kupokea wafanyakazi sio lazima hela tu kuwe na maandalizi,”amesema.

Amefafanua maandalizi hayo ni nyumba ambayo mfanyakazi ataishi hata kama atatakiwa kulipia mwenyewe.

Sitta amesema jimbo lake lina uhaba wa walimu zaidi 600 katika shule za msingi na sekondari.

Amesema walimu wanapokuwa wengi inakuwa vigumu kwa Tume ya Utusmishi wa Walimu kuwashughulikia.

Amesema kutokana na hilo Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (Usemi) imetaka kufanyika kwa tathimini kwa tume hiyo kwasababu ya wingi wa walimu na maeneo wanayofanyia.

Amesema lengo ni kuichunguza iwapo inafanya kazi iliyokusudiwa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments