TIMU YA TAIFA YA WASICHANA YAWEKA KAMBI YA SIKU 10 MANISPAA YA BUKOBA

 

Timu ya Taifa ya Wasichana chini ya miaka 17 wakifanya mazoezi katika uwanja wa Mpra wa miguu wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba


Katibu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Kagera (KRFA) Bw. Amin Abdul amesema kuwa wamepokea Timu ya Taifa ya wasichana wenye umri wa chini ya miaka 17, ambayo imeweka kambi ya siku 10 katika Manispaa ya Bukoba ikiwa ni maandaliz ya mchezo wa baina ya timu hiyo na timu ya wasichana wenye umri huo, ya nchini Burundi.

Bw. Abdul amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika uwanja wa Mpira wa miguu wa Kaitaba na kwamba timu hiyo imeweka kambi mkoani humo kutokana na hali ya hewa kuendana na ya nchini Burundi, ambapo mchezo huo utafanyika Nchini Burundi.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Wasichana chini ya miaka 17 Bakari Shime amesema kuwa wapo katika mazoezi ya kuelekea mchezo baina yao na Timu ya Taifa ya Wasichana chini ya miaka 17 Nchini Burundi itakayofanyika Mjini Ngozi tarehe 16 mwezi huu.

Amesema kuwa kuwekwa kwa kambi hiyo katika mkoa wa Kagera ni moja ya mkakati wa kusaka ushindi katika mechi hiyo, ambayo ni moja ya tiketi ya kutafuta nafasi ya kufuzu kucheza kombe la dunia, na kuwaahidi Watanzania ushindi.
Na Mbuke Shilagi Kagera.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments