Uhaba wa Mafuta Ya Petroli Wawalazimisha Wakenya Kwenda Tanzania Kuyatafuta


Uhaba wa mafuta ya petroli katika Kaunti ya Kwale, Pwani ya Kenya umewalazimisha madereva kusafiri hadi katika nchi jirani ya Tanzania kupitia mpaka wa Lungalunga ili kutafuta bidhaa hiyo muhimu, huku wafanyabiashara wakipandisha bei kutokana na uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo nchini Kenya.

Kwa mujibu wa gazeti la Taifa Leo, vituo vingi vya mafuta katika miji ya Kwale na Ukunda huko Pwani ya Kenya vimekumbwa na ubaha mkubwa wa dizeli na petroli.

Bidhaa hiyo ilipatikana tu katika vituo vikubwa vya mafuta katika kaunti za mpakani. Foleni ndefu pia zilikuwa zimepangwa hasa nyakati za asubuhi na jioni wakati madereva wa magari walikimbilia kujaza mafuta kwenye magari yao.

Abdalla Kalama, dereva wa Tuktuk huko Ukund amenukuliwa akisema, "Tumeambiwa kuwa kuanzia kesho, kunaweza kusiwe na mafuta ndiyo maana nataka kuhakikisha najaza tanki langu ili niendelee kufanya biashara."

Ramani inayoonesha mpaka wa Kenya na Tanzania

Hali hiyo pia imevuruga shughuli za uchukuzi na usafiri katika maeneo ya mijini katika kaunti hiyo ya Pwani ya Kenya kama vile Ukunda, ambapo nauli zimepanda. Madereva wa magari nchini Kenya sasa wanatutumia mpaka wa Lungalunga kwenda kusaka mafuta kwa bei nafuu nchini Tanzania.

Mgogoro wa Ukraine na vikwazo vya Magharibi dhidi ya Russia vimepelekea nchi nyingi duniani kukumbwa na ubaha au ukosefu wa mafuta ya petroli, na vilevile chakula. 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments