Ujenzi SGR Makutupora-Tabora Kukamilika Miezi 42

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Makutupora-Tabora utagharimu Sh4.606 trilioni huku ukitarajiwa kutumia miezi 42 ikiwemo miezi minne ya majaribio.

Treni zitakayotumia reli hiyo zitakuwa na mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa ambapo zitatumia saa sita kutoka Dar es Salaam hadi Tabora kwa treni ya abiria huku za mizigo zikitembea kilometa 120 kwa saa.

Kadogosa amesema hayo leo Jumanne Aprili 12, 2022 katika uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa reli hiyo unaofanywa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Profesa Makame Mbarawa.

Amesema makadirio ya majaribio yanategemea kuwa muda wa chini sana utakuwa miezi minne, lakini yanaweza kwenda hadi zaidi ya miezi hiyo.

“Kwa hiyo tunategemea mradi huu unaoanza saa hizi, utakamilika Oktoba 2025, hii inajumuisha usanifu na ujenzi kwa mkandarasi. Wakati anasanifu kuna baadhi ya nyumba zitapitiwa ila wote watapatiwa haki zao,”

Amesema mkandarasi amashapewa aina ya reli ambayo inayohitaji na si yeye kuleta kile ambacho hakitakiwi.

“Itakuwa na vivuko vya kutengenisha reli na barabara kwa kuondoa muingiliano wa barabara na reli, hii ikiwa na maana kuwa ikiwa yeye atakuwa chini treni itapita juu au yeye akiwa juu treni itapita chini jambo hili litafanya usalama kuwa wa juu”

Amesema katika ujenzi huo, madaraja makubwa 32 yanatarajiwa kujengwa na vivuko vya juu 12 na vya chini 15 huku vivuko vya watembea kwa miguu, mifugo na wanyama vikiwa 49.

“Vivuko hivi vinamaana kwa sababu reli hii haitaruhusu mtu kupita juu kwa ajili ya usalama, tutazungushia wigo reli yote,”

Treni hiyo itakapoanza kazi itakuwa na vituo nane Manyoni, Itigi, Kazikazi, Tula, Malongwe, Gaweko, Igalula na Tabora.

“Niwaambie tu, hatujengi stesheni hapa Tabora, tutajenga ‘shopping mall’, sehemu ya maduka makubwa, migahawa, tutakuwa na sehemu ya wafanyabiashara wadogo. Nina imani kuwa pale ndiyo itakuwa sehemu mnakutania,” amesema Kadogosa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments