Magenge ya wabeba silaha Ituri |
Taarifa ya OCHA imeeleza kuwa: Kwa akali raia 20 waliuawa mapema leo (jana Jumatatu Aprili 11) kufuatia shambulizi la wabeba silaha katika mji wa Mangusu, eneo Irumu. Washambuliaji walipora pia nyumba na maduka katika miji jirani ya Bavonkutu na Bandiboli.
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limebainisha kuwa, mbali na watu 20 kuuawa jana, wengine zaidi ya 40 wameuawa ndani ya siku saba zilizopita katika eneo la Irumu mkoani Ituri, kaskazini mwa DRC.
Watu wasiopungua 60 wameuawa katika mashambulizi ya magenge ya wabeba silaha kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. |
Ripoti mbalimbali za vyombo vya habari zinaarifu kuwa, watu zaidi ya milioni 1.9 katika mkoa wa Ituri wamelazimika kuwa wakimbizi mkoani Ituri, kutoka na hujuma hizo za magenge ya wabeba silaha.
0 Comments