CCM Arusha Kumenoga! Ndivyo unavyoweza kuelezea hali ilivyo kutokana na maandalizi yanayondelea katika ukumbi wa mikutano wa Mount Meru jijini Arusha ambako Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Abdulrahman Kinana akitarajia kuzungumza na maelfu ya wana CCM katika mkoa huu.
Mandalizi kwa ajili ya mkutano huo wa Kinana ambaye ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka yamekamilika . Kwa hali ilivyo ukumbini unaweza kusema Arusha hawana jambo dogo na wamejipanga vilivyo kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa.
Wana CCM kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Arusha wakiwemo na viongozi wa Chama na Serikali nao watakuwepo kwenye kikao kazi hicho cha Makamu Mwenyekiti wa Chama ambaye alichaguliwa kwa kura nyingi na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.
Kwa kukumbusha tu Kinana leo atahitimisha ziara yake aliyoanza kuifanya Mkoa wa Pwani,Tanga,Kilimanjaro na leo anamalizia katika Mkoa wa Arusha.Tangu jana alipoingia Arusha amepata mapokezi makubwa ,mapokezi ya heshima.
Kinana alipoingia na kupokelewa na wana Arusha alipata nafasi ya kusalimia ambapo aliwaambia wananchi hao anawashukuru kwa mapokezi makubwa na kwamba anawapenda sana.Aliwasili Arusha jana Alasiri na ilipofika jioni alipata nafasi ya kufuturu na wananchi wa mkoa huo.
Kwa siku ya leo katika ukumbi wa mikutano Mount Meru wana CCM wanasubiri kwa hamu kubwa kumsikiliza Kinana huku wengi wakionesha bashasha kubwa hasa kwa kuzingatia Kinana anatoka katika Jiji la Arusha na amewahi kuwa mbunge wako kwa kipindi cha miaka 10. Michuzi TV na Michuzi Blog itaendelea kukujulisha matukio yatakayokuwa yakijiri ukumbini.
Na Said Mwishehe
0 Comments