MANYONI MKOANI SINGIDA YAFIKIA ASILIMIA 90 YA ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge akizungumza na wakuu wa idara wa mkoa huo na  viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakati alipokuwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Singida ya Solya aliyoifanya leo wilayani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge na Mhandisi wa Wilaya ya Manyoni, Ahmed Suleiman wakiangalia ramani ya shule hiyo ya sekondari.
Ukaguzi wa ujenzi wa jengo la dharura na jengo la wagonjwa mahututi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida  Mandewa ukifanyika.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Mandewa, Deogratias Manuba (kushoto) akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa majengo hayo.
Muonekano wa ujenzi wa majengo hayo.
Ukaguzi ukiendelea.


Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida  Mandewa, Deogratius Manuba akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Mahenge wakati akimuonesha vifaa tiba vilivyopokelewa kwenye hospitali hiyo..
Vifaa tiba vilivyopokelewa.
Ukaguzi wa ujenzi wa mnara wa kuwekea matenki ya kuhifadhia maji unaojengwa kwa fedha za ndani za hospitali hiyo ukiendelea.
Dk.Mahenge akizungumza na wafanyakazi wa hospitali hiyo baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali.
Ukaguzi ukiwa tayari umekamilika.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa akitoa taarifa ya zoezi la Anwani za Makazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge. Kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Victorina Ludovick na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Melkzedeki Humbe .

Dk.Mahenge akisisitiza jambo wakati akizungumzia zoezi la Anwani za Makazi na Postikodi.
Katibu wa Kamati ya Ufatiliaji Operesheni Anwani za Makazi Mkoa wa Singida ambaye pia ni Afisa TEHAMA, Athumani Simba akitoa ufafanuzi kuhusu zoezi hilo kwa mkuu wa mkoa.
Safari ya ukaguzi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Singida ya Solya ikifanyika.
  Mkururgenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Melkzedeki Humbe (kulia) akimuelekeza jambo, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya Solya. Katikati ni Mhandisi wa Wilaya ya Manyoni, Ahmadi Suleimani.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Manyoni imefikisha asilimia 90 ya zoezi la anwani za makazi na postikodi licha ya kuwepo changamoto ndogondogo zilizojitokeza.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Rahabu Mwagisa wakati akitoa taarifa ya zoezi hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge alipokuwa katika ziara ya kukagua zoezi hilo aliyoifanya leo wilayani humo.

"Tulikuwa na changamoto ya ukasanyaji wa  takwimu wakati wa uhainishaji wa hesabu ambapo awali tulipata idadi ya anwani za makazi 99,930 lakini baada ya kufanya masahihisho ya makadirio ya anwani tumebaini idadi kamili ni 42,000 kama zilizowasilishwa awali na watendaji wa kata ambao walihesabu idadi ya kaya badala ya anwani na katika utekelezaji ilibainika  kwamba kaya zaidi ya moja kuwa ndani ya anwani moja na kupelekea idadi ya anwani kuwa chache kuliko makadirio" alisema Mwagisa.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo Dk.Mahenge aliitaka halmashauri hiyo  kuhakikisha zoezi hilo linakamilika kabla ya muda uliopangwa ili kwenda sambamba na wilaya zingine ambapo alitumia nafasi hiyo kuwapongeza viongozi wote kwa uchapaji kazi mzuri.

"Mkuu wa wilaya, mkurugenzi, mwenyekiti wa halmashauri, watumishi na wataalam wote kwa ujumla nitumie nafasi hii kuwapongezeni kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa kushirikiana na wananchi na watendaji wenu" alisema Mahenge.

Dk. Mahenge alisema alisema zoezi hilo kimkoa limefikia asilimia 84.82 huku anwani za makazi zilizohesabiwa Singida Manispaa zikiwa ni 47,952, Ikungi 55,765, Iramba 55,686, Singida DC 50,672, Mkalama 45,039 na Itigi 35,000.

Wakati huo huo Dk. Mahenge amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya Luba Contractors CO.LTD ambayo imepata kazi ya kujenga jengo la wagonjwa mahututi na ujenzi wa wodi ya dharura (EMD) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ya Mandewa kukutana naye Aprili 25, 2022 ili kujadili kusuasua kwa ujenzi wa majengo hayo ambayo licha ya kupewa fedha bado ujenzi wake haujafika hata kiwango cha lenta huku kukiwa na sababu mbalimbali.

"Katibu Tawala nahitaji kuonana na mkandarasi mwenyewe hapa eneo la mradi ili tujadili atamalizaje hii kazi ndani ya muda aliopangiwa vinginevyo tutamnyang'anya huu mradi na kumpa mtu mwingine na pia tuna uwezo wa kumzuia hasipate kazi mahali popote hapa nchini" alisema Mahenge akioneshwa kukerwa na ucheleweshwaji wa ujenzi wa majengo hayo.

Aidha Mahenge alimtaka msimamizi wa ujenzi wa mradi huo kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ukizingatia kuwa amewekewa taa kwa ajili ya kazi hiyo.

Katika ziara hiyo pia Dk.Mahenge alitembelea na kukagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mkoa ya Wasichana ya Solya ambao ujenzi wake utagharimu Sh. 3. Bilioni ambayo inajengwa wilayani Manyoni.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments